OnlineThursday, November 3, 2016

TTCL NA HUAWEI WAZINDUA MTANDAO WA 4.5 G

 


Kampuni ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ya Huawei Tanzania na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) zimeungana na kuzindua mtandao wa 4.5 utakaokuwa wa kwanza kwa mitandao yote nchini Tanzania.

Mkurugenzi Mtendaji wa Huawei Tanzania Bruce Zhang amesema uzinduzi huo unadhihirisha mafanikio ya TTCL kwenye safari ya mabadiliko ya kukua kibiashara nchini.

Hivi karibuni serikali ya Tanzania ilitangaza kumiliki hisa zote za TTCL baada ya kuchukua asilimia 35 zilizokuwa zinamilikiwa na Kampuni ya Bhart Aitel.

DAR ES SALAAM:RAIA WATATU WA PAKSTANI WAHUKUMIWA KWA KOSA LA KUMILIKI MITAMBO YA MAWASILIANO BILA LESENI

Raia watatu kutoka Pakstani wamehukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kulipa faini ya shilingi milioni 120 na iwapo watashindwa watatumikia kifungo cha mwaka mmoja jela kutokana na kosa la kula njama,kuingiza nchi Tanzania vifaa vya kielektroniki vya mawasiliano bila kuwa na leseni ya TCRA,kuvisimika,kuendesha huduma za mawasiliano ya simu za kimataifa bila kibali kutoka TCRA,kukwepa malipo na kusababishia serikali na mamlaka hiyo hasara ya shilingi milioni 140,049,000.

Raia hao wa Pakstani ni Hafeez Irfan (32),Mirza Baig (41) na Irfan Baig (46) na wakidaiwa kutenda makosa hayo katika Hoteli ya Butterfly iliyoko Kariakoo,Wilaya ya Ilala katika chumba namba 905.