OnlineThursday, October 29, 2015

TWEET MBILI ZA DR JOHN POMBE MAGUFULI KABLA NA BAADA YA KUTANGAZWA KUWA RAIS WA TANZANIA WA AWAMU YA TANODr John Pombe Magufuli leo Oktoba 29,2015 alitweet kwenye account yake ya twitter ya https://twitter.com/MagufuliJP  @MagufuliJP
kabla ya kutangazwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, miongoni mwa wagombea 8 waliokuwa wakigombea nafasi hiyo katika uchaguzi Mkuu wa Tanzania uliofanyika Oktoba 25,2015

Katika account yake Dr John Pombe Magufuli ambaye anakuwa Rais wa Tanzania awamu ya tano alitweet kwa mara ya mwisho Oktoba 24 ukiondoa zile alizoretweet za account ya twitter ya chama chake cha Siasa.

Saturday, October 17, 2015

POLISI NCHINI UJERUMANI WAONYA WAZAZI WANAOWEKA PICHA ZA WATOTO FACEBOOKPolisi nchini Ujerumani wameonya wazazi dhidi ya kuweka picha za watoto wao hadharani katika mtandao wa kijamii wa Facebook.

Katika ujumbe kwenye ukurasa wao wa Facebook, polisi wa eneo la Hagen wametahadharisha wazazi kuwa picha hizo zinaweza kunakiliwa au kubadilishwa na kutumiwa vibaya na watu wanaovutiwa kimapenzi na watoto.

 Aidha, watoto wahusika huenda wasipendezwe na picha hizo kuwa wazi mitandaoni watakapokomaa na kuwa watu wazima. Wazazi wameshauriwa kuhakikisha kuwa picha hizo, ikilazimu, zinatazamwa na marafiki zao pekee na si kila mtu mtandaoni.
Ushauri huo wa polisi hao umeenezwa sana mtandaoni na kuvutia hisia mseto. Afisa msemaji wa Polisi wa Hagen ameiambia BBC kwamba walishangazwa na jinsi ujumbe huo wa tahadhari ulivyopokelewa. Amesema wanakadiria kuwa umesomwa na watu zaidi ya milioni 12.

Bw Hanki ameongeza kuwa ujumbe huo haujaongozwa na matukio yoyote mapya ya kesi za uhalifu au watu wanaovutiwa na watoto kimapenzi huko Hagen.


Picha zilizobadilishwa

Shirika la kujitolea linalohusika na ulinzi wa watoto NSPCC katika taarifa yao wamesema: " Wazazi wote wanapaswa kujisikia huru na kufurahia kuchukua picha za watoto wao na kushirikiana nao na marafiki na familia. Hata hivyo, tunapaswa wote kuwa makini wakati wa kuziweka picha hizo mitandaoni.

"Tunajua kwamba wahalifu wa ngono wana uwezo wa kubadilisha picha za watu wasiokuwa na hatia, na maendeleo katika programu za kuhariri picha zimefanya hili kuwa rahisi sana.

" Hivyo kama wazazi watachapisha picha za watoto wao kwenye mitandao, wanapaswa kuchukua hatua ili kuhakikisha kwamba wanachunguza hali yao ya faragha na kuhakikisha wanaridhishwa na watu watakaotazama picha hizo."

Shirika hilo limeongeza kuwa iwapo wazazi wana wasiwasi kuwa picha ya mtoto wao imeanguka mikononi mwa watu wabaya, wanapaswa kuwasiliana na Internet Watch Foundation, Child Exploitation na Online Protection Centre (Ceop) au kuwasililiana na NSPCC kupitia numbari ya msaada ya simu ya 0808 800 5000 ambapo watapokeza usaidizi.

Tuesday, October 13, 2015

DAR ES SALAAM :TTCL WALIVYOZINDUA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (kulia) akikata keki katika moja ya tawi la ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam kuzinduwa wiki ya huduma kwa wateja. Kampuni ya simu ya TTCL leo imezinduwa wiki ya huduma kwa wateja ambayo ilianza Oktoba 12 hadi 16, 2015.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura akisaini kitabu cha wageni katika moja ya tawi la ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam kwenye hafla ya uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja. Kampuni ya simu ya TTCL leo imezinduwa wiki ya huduma kwa wateja ambapo inaanzia Oktoba 12 hadi 16, 2015.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura akisalimiana na mmoja wa wateja waliofika kupata huduma katika tawi la ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam lililopo Makao Makuu ya kampuni hiyo, kabla ya kumlisha keki kwenye hafla ya uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (kushoto) akimlisha keki mmoja wa wateja wa kwanza waliofika kupata huduma katika moja ya tawi la ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam kwenye hafla ya uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja. Kampuni ya simu ya TTCL imezinduwa wiki ya huduma kwa wateja ambapo ilianza Oktoba 12 hadi 16, 2015.


Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (kushoto) akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja leo jijini Dar es Salaam. Kampuni ya simu ya TTCL imezinduwa wiki ya huduma kwa wateja ambapo inaanzia Oktoba 12 hadi 16, 2015.


Meneja wa Kanda ya TTCL Dar es Salaam Kati, Jane Mwakalebela (kushoto) akimlisha keki Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura kwenye hafla ya uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja.
Ofisa Mkuu wa Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota akifafanua jambo kwa wageni waalikwa kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja  jijini Dar es Salaam.
Hapa ni wakati wa kugonganisha glasi za mvinyo kutakiana afya njema na utendaji bora...! 
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (kulia) akitoa zawadi kwa mmoja wa wateja wa kwanza waliofika kupata huduma katika moja ya tawi la ofisi za kampuni hiyo leo jijini Dar es Salaam kwenye hafla ya uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja.

Baadhi ya wateja wa kwanza wa TTCL waliofika kupata huduma leo katika matawi ya huduma kwa wateja ya jijini Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja na zawadi zao na Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kazaura (katikati) kwenye hafla ya uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja.

Akizungumza na baadhi ya wateja wa TTCL, maofisa na wafanyakazi jijini Dar es Salaam Mkuu wa Idara ya Huduma kwa Wateja TTCL, Laibu Leonard alisema ndani ya maadhimisho hayo maofisa wa TTCL watapita kuwatembelea wateja ofisini na majumbani kuwasikiliza maoni yao ikiwa ni pamoja na kupata mrejesho juu ya huduma wanazozitoa. 


Alisema maofisa waandamizi wa kampuni hiyo watashiriki moja kwa moja katika zoezi hilo la kutoa huduma pamoja na kuwatembelea wateja kupata maoni yao na pia kutoa shukrani kwa wao kukubali kuhudumiwa na kampuni hiyo ya simu ya kizalendo nchini Tanzania. 

 "...Mbali na kutoa huduma zetu katika matawi mbalimbali katika kipindi hiki maofisa waandamizi wa TTCL watawatembelea wateja moja kwa moja katika ofisi zao au majumbani kwa ajili ya kuwasikiliza na pia kupokea naoni yao," alisema Leonard akizungumza katika hafla hiyo. 

Katika uzinduzi wa hafla hiyo TTCL ilitoa zawadi kwa wateja watano wa mwanzo waliofika katika vituo vya huduma kwa wateja leo asubuhi kuhudumiwa na kampuni hiyo pamoja na kuwazawadia maofisa wa TTCL waliofanya vizuri zaidi katika idara ya huduma kwa wateja ya kampuni hiyo, ikiwa ni motisha ya kuchochea utendaji bora zaidi. *Imeandaliwa na www.thehabari.com

Saturday, October 10, 2015

IFAHAMU NJIA MADHUBUTI YA KUKABILIANA NA UHALIFU MTANDAO


Tukio la kipekee katika anga ya usalama mitandao ambalo limekualiki azimishwa kila mwaka katika mwezi wa Oktoba ambapo mataifa yanaadhimisha siku ya uelewa wa maswala ya usalama mitandao duniani kote. Na imani Mwaka huu Tanzania itauchukulia mwezi huu kinamna ya kipekee ili kuweza kukuza uelewa kwa watu wake Tukio ambalo nategemea makampuni mbali mbali na maeneo mengine yataandaa program mbali mbali za kukuza uelewa wa maswala ya usalama mitandao ili kuweza kufikiwa malengo yaliyokusudiwa na wanausalama wote mitandao duniani kote.
Aidha, inaaminika kama ilivyo katika uhalifu mwingine wowote ni vigumu kumaliza kabisa tatizo ila kuna njia kadhaa ambazo kwa umoja wake zikifanyiwa kazi vizuri zinaweza kabisa kupunguza kwa kiasi kikubwa sana tatizo la uhalifu mtandao.

 Tatizo kubwa kubwa ni kuwa njia hizi zimekua zikiishia katika maandishi baada ya kujadiliwa na wanausalama mitandao ambapo mimi binafsi nilikua miongoni mwao.

 Kwa kupata elimu hii wale wote waliokua wakifanya uhalifu mtandao pasi na kujua wanakua na ufahamu wa kutosha na hatimae kundi hili linakua limeondokana na uhalifu mtandao. Aidha, kundi la pili ambalo ni lile linalofanya uhalifuu huu wa mtandao wakiwa hawana namna kwa kutokujua athari zake baada ya kujua athari za uhalifu mtandao kwao na kwa wengine na pia kujua njia mbadala wanazoweza kutumia kuepukana na uhalifu huu kupitia elimu ya uelewa ya usalama mitandao kundi hili linaweza pia likapunguzwa hadi asilimia 84% kwa mujibu wa wataalam wa usalama mitandao.Kundi la mwisho ambalo ni wahalifu wanaofanya uhalifu huu makusudi ingawa wanajua wakifanyacho na hawana utayari wa kuepukana na uhalifu huu mtandao nalo linapunguzwa nguvu kwani watumiaji mitandao wanakua na uelewa wa namna wahalifu hawa wanavyo fanya uhalifu na njia sahihi za kujilinda hatimae kundi hilipia linakosa watu wengi wanaoweza kuingia katika mtego wao wa uhalifu mtandao na kupungukiwa kasi na nguvu ya usambazaji wa uhalifu huu.Inaaminika asilimia zaidi ya 37% ya wahalifu wa kundi hili la tatu wanapokosa watu wanoweza kuingia mtegoni wanajikuta wanakata tama na kujishughulisha na mambo mengine tofauti na uhalifu mtandao.Kumekua na wimbi kubwa la makampuni mengi mbali na kua na teknolojia nzuri ya kuzuia uhalifu mtandao bado yameendelea kugubikwa na uhalifu mtandao kutokana na kutowekea mkazo swala hili la kukuza uelewa wa maswala haya ya usalama mitandao. Pia mataifa mengi yameendelea kujipanga kwa kua na vitengo kadhaa vya udhibiti uhalifu pamoja na kua na sharia sahisi za kudhibiti uhalifu huku bado wimbi kubwa la wahalifu mtandao bado likiendelea kua kubwa.

Tatizo ni kukosekana na njia sahihi na namna madhubuti ya kuendea njia hii ya kukuza uelewa wa maswala ya usalama mitandao ambapo kama nilivyo fafanua awali ingeweza kabisa kupunguza kwa kiasi kukubwa swala hili la uhalifu mtandao.Kumekua na jitihada nyingi za kuhamasisha kuanzia ngazi ya mtu binafsi, Makapuni , Nchi, Bara na hatimae Dunia nzima kujenga tamaduni ya kukuza uelewa wa matumizi salama ya mitandao ili kukabiliana na wimbi kubwa la uhalifu unaoendelea kukua kwa kasi hivi sasa.Swali linaloulizwa ni kwamba pamoja na jitihada nyingi  za wanausalama mtandao ambapo hadi sasa pamoja na mambo mengine, tayari kuna mwezi wa Kumi ambao unafahamika kama mwezi maalum wa maswala ya uelewa wa usalama mitandao yaani “OCTOBER" – Cybersecurity Awareness Month”  na kupatikana kwa tamthilia maalum ambazo zipo kukuza uelewa wa usalama mitandao.Jibu ni kwamba, Jitihada hizi zimebaki kwa wanausalama mitandao na wananchi wakawaida bado imekua ni vigumu sana kufikiwa na kuelewa pamoja na kua miongoni mwa jitihada hizi.Wengi bado wamebaki wakijua swala la ufahamu na uelewa wa maswala ya usalama mitandao ni swala la wanausalama mitandao pekee huku wengine wakiamini pia wana TEKINOHAMA ndio pia wanausika.Inasahaulika kabisa swala la kubaki salama kimtandao ni swala linalo takiwa kuanzia katika ngazi ya mtu binafsi sawa kabisa na swala la ulinzi wa uhalifu mwingine wowote. Tumekua na utamaduni wa pamoja na mambo mengine, kufunga milango, kuwa na walinzi katika nyumba zetu na kuweka taa za nje tukiamini zinauwezo wa kusaidia upungufu wa uhalifu majumbani mwetu.Cha kushangaza zaidi, Jitihada hizi binafsi huzioni zikiamishiwa katika udhibiti wa uhalifu huu wa mitandao ambapo vitu kama Antiviruses, Maneno ya siri na mengineyo ni ya kuanzia katika ngazi ya mtu binafsi.Kuna Kila namna ya kufahamu kua pale swala la uelewa wa maswala ya usalama mtandao litakapoweza kufanyiwa kazi kwa kiwango kizuri basin i wazi kabisa linaweza kusaidia kila mmoja kuelewa na kuhimili ipasavyo uhalifu huu mtandao katika ngazi ya mtu binafsi, pamoja na kukuza utamaduni wa kila mmoja kujua anajukumu ssi tu la kujilinda binafsi kimtandao bali na kulinda wengine ipasavyo kuhakiki taifa, bara na hatimae dunia inabaki salama kimtandao.Kwa ufupi nimefafanua kwa kina faida zinazoweza kupatikana pale uelewa sahihi wa elimu ya usalama mtandao itapatikana kwa jamii zetu na katika maofisi yetu (Makampuni) Maelezo hayo yanawea kusomeka kwa ku “BOFYA HAPA” Wakati huo huo nilipozungumzia mambo muhimu yanayo paswa kuenda sambamba na uwepo wa sharia mpya ya usalama mitandao niliainisha kwa kina swala la uelewa sahihi wa maswala ya usalama mitandao pamoja na ujuzi wa kufanyia kazi uchunguzi wa uhalifu mtandao na ushirikiano kama inavyoweza kufatiliwa katika video hii hapo chini.
 


Leo nitaangazia njia ambayo imeshika nafasi ya juu na imeonekana na uwezo mkubwa wa kuhimili uhalifu mtandao ambapo imeaminika inauwezo wa kupunguza aina mbili za wahalifu mtandao pamoja na kusababisha aina ya tatu kupungua makali. Kwa ujumla wake imezungumzwa inaweza kupunguza hadi asilimia 71% ya uhalifu wote mtandao kama itafatwa vizuri na kupewa uzito wa kipekee katika mataifa yote.


Njia hii si nyingine bali ni “Awareness Program” Yaani elimu ya uelewa wa uhalufu mtandao na namna ya kujilinda. Elimu hii inatoa fursa kwa mwananchi wa kawaida kutambua aina mbali mbali za uhalifu mtandao, athari zake, njia ya kujilinda, Na Namna ya kulinda wenzake.

 Natoa wito kwa kila mmoja wetu kukuza upendo wa kufatilia na kutaa kujua namna mbali mbali za kuweza kujilinda katika ngazi ya mtu binafsi na uhalifu huu mitandao unaokua kwa kasi zaidi hivi sasa huku makampuni kua na tamaduni ya kuwa na mafunzo maalum ya maswala haya na taifa kwa ujumla kuhakiki linaongeza jitihada katika kukuza uelewa kwa wananchi katika maswala ya usalma mitandao ili kukabiliana na ongezeko la uhalifu mtandao nchini.
 Na:Yusuph Kileo

ANAYETUHUMIWA KUENEZA TAARIFA ZA UONGO KWENYE MITANDAO YA KIJAMII KUHUSU MKUU WA MAJESHI NCHINI TANZANIA AFIKISHWA MAHAKAMANI


Serikali ya Tanzania imemfikisha Mahakamani Bernedict Angelo Ngonyani kwa tuhuma za kutumia mtandao wa Facebook na WhatsApp kueneza taarifa za uongo kuwa mkuu wa majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange amelazwa Nairobi kwa madai ya kulishwa chakula chenye sumu.

Akizungumza kwenye eneo la mahakama ya kisutu jijini Dar es Salaam ambako mtuhumiwa huyo alifikishwa kwa ajili ya kusomewa mashitaka, wakili mkuu wa serikali Joanes Karungura amesema, mtuhumiwa huyo amefikishwa mahakamani hapo kwa kuvunja kifungu namba 16 cha Sheria ya Makosa ya Kimtandao ya mwaka 2015.

Sheria hiyo ijulikanyo kwa lugha ya Kiingereza, Tanzania Cybercrime Act 2015, inakataza kusambaza ujumbe, taarifa au data za uongo au zisizothibitishwa kwa njia ya mtandao.

Ngonyani ambaye amenyimwa dhamana kutokana na aina ya kosa alilofanya la kuvunja sheria ya mtandao ya mwaka 2015 alikamatwa Septemba 25 mwaka huu kwa ushirikiano wa mamlaka ya mawasiliano nchini, Jeshi la Polisi na vyombo vya ulinzi na usalama.

Wakati huo huo serikali imewafikisha watuhumiwa watano katika mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam, mmoja raia wa Afrika ya Kusini, mmoja raia wa China na watatu kutoka Pakstani, kwa kosa la kuiba kwa njia ya kimtandao wizi wenye thamani ya karibu shilingi billion moja, fedha za Kitanzania.

Mhandisi wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini, TCRA anasema watuhumiwa hao walikutwa na laini zaidi ya mia moja zenye usajili bandia ambazo walikuwa wanazitumia kufanya biashara ya kupiga simu Kimataifa kinyume cha sheria.

Mtuhumiwa wa makosa ya mtandao Benedict Angelo Ngonyani (24) (wa kwanza kulia) anayetuhumiwa kusambaza taarifa za uongo zinazomhusu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, akiwa katika mahakama ya hakimu mkazi ya Kisutu akisubiri kusomewa mashitaka.
Wengine ni watuhumiwa wa wizi kwa kutumia mitandao ya simu (fraud and use of telecommunication network) Ally Hamze (53) raia wa Afrika Kusini (wa pili kulia), Huang Kun Bing (26) Raia wa China (wa tatu kulia) Irfan Mirza Baig (46) (wa kwanza kushoto) Hefeez Irfan (32) (wa pili kushoto) na Mirza Rizwan Baig (41) (wa tatu kushoto) wote watatu raia wa Pakistani wakiwa katika Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu wakisubiri kusomewa mashitaka ya wizi kwa kutumia mitandao ya simu (fraud and use of telecommunication network). 

Kesi zote zimeahirishwa hadi Oktoba 23 mwaka huu na watuhumiwa wote wamepelekwa rumande huku uchunguzi ukiendelea.

Thursday, October 8, 2015

CONNECTMOJA TECHNOLOGIES LIMITED WAZINDUA MFUMO MPYA WA SCHOOL MANAGEMENT SYSTEM

Kampuni ya Connectmoja Technologies  inayoendesha shughuli zake hapa nchini Tanzania leo imezindua Mfumo madhubuti unaojulikana kwa jina la  KSchool  Management system.


Akizungumza na wana habari, Mtaalamu wa utafiti na ukuzaji wa Masoko Bw. Fred Crich amewaambia wanahabari kwamba Kampuni yao ya ConnectMoja Technologies  imejikita zaidi katika kuhakikisha inasaidia sekta ya elimu na uwekezaji kukua pamoja na maendeleo ya Teknolojia hapa Nchini.Bw. Crich amesema mfumo  huu umewalenga wamiliki wa mashule kwani mfumo unawawezesha kuweka rekodi sahihi za wanafunzi, kutunza kumbukumbu za mienendo ya wanafunzi, kuweka rekodi ya matokeo ya wanafunzi na wazazi pia wanaweza kuona rekodi hizi wakiwa majumbani au mahala popote kwa kutumia simu za kiganjani au computer zenye internet.

Mfano. Mwanafunzi  anapotoka shule, Mzazi atakuwa na uwezo wa kuingia kwenye  mfumo huu kupitia(Parent Portal) na kujua kama mtoto alifika shuleni, na kama alifika alifundishwa nini, pia kujua kama ana Homework ya kufanya pindi afikapo nyumbani, pia itamwonesha matokeo yake papo hapo.

Mfumo huu una Teachers Portal na students portal ambapo Mwalimu anaweza kutuma Assignments kwa wanafunzi hata wakiwa Likizo.
Bw. Crich ameelezea kwamba mfumo huu umeanza kutumika kwenye baadhi ya shule hapa Nchini na kwa sasa wameuboresha zaidi ili uweze kuwanufaisha wazazi pamoja na wadau wa sekta ya elimu.

Pia anakaribisha wamiliki wa shule wote  wanaotaka kuupata mfumo huu, bei ni nafuu .

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia:
call: +255 777 88 0000 7  au  0714 215 600

TIGO YAENDELEA KUSHEREKEA JUMA LA HUDUMA KWA WATEJAMeneja wa duka la TigoNkurumah, Lulu Kikuli  akimkabidhi zawadi  ya simu Grace Joachim mkazi wa Tandale  ikiwa ni  sehemu maadhimisho  ya wiki ya wateja wa
Tigo
Mwandishi wa habari wa TV1 Robert Latonga akifanya mahojiano na  mteja wa  Tigo, Hamadi Maliwata  mkazi wa Mbagala kwenye maadhimisho  ya wiki ya  wateja wa  Tigo
Meneja wa Duka la Tigo Nkurumah, Lulu Kikuli  akifanyiwa mahojiano na Mwandishi wa habari   wa TV1 Robert Latonga


Meneja wa ubora  huduma  kwa wateja  wa  Tigo Bi. MwangazaMatotola, akimkabidhi  fulana  mteja wa  Tigo  Nickson Mbwambo  mkazi wa  Mabibo, 
 Mtaalam wa huduma kwa wateja wa Tigo Jackson Jerry(kushoto),  
, Halima Kasoro (katikati) na
Meneja wa ubora huduma kwa wateja wa Tigo Mwangaza Matotola(kulia) wakiwa
kwenye picha ya  pamoja


Mteja  wa   Tigo  Zenah   Hamdi mkazi wa  Tandika, akipata   huduma toka kwa Mtoa huduma wa   Kampuni ya Tigo

Thursday, October 1, 2015

KIONGOZI WA KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO ULIMWENGUNI TED N.C.WILSON AJIUNGA NA FACEBOOK NA TWITTER KWA AJILI YA KUWASILIANA NA WAUMINI NA WATU MBALIMBALITed Wilson na mkewe Nancy

Kiongozi wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Ulimwenguni Ted N.C. Wilson ameziundua rasmi mawasiliano yake kwa njia ya mitandao ya kijamii ya facebook na twitter alhamisi Oktoba 1,mwaka huu ili kuwasiliana moja kwa moja na waumini wa kanisa hilo pamoja na watu mbalimbali.

Wilson anasema atatumia wasifu wake wa twitter kwa anuani yake ambayo ni  @pastortedwilson  na kwenye mtandao wa facebook anatumia ukurasa wake ambao ni facebook.com/pastortedwilson  ambapo atakuwa akiwasiliana na watu kwa njia ya maombi,mafundisho ya Biblia na Roho ya Unabii,taarifa zake za utume,picha na habari mbalimbali za ziara zake za kikazi.

Sikiliza ujumbe wa ukaribisho wa Kiongozi huyo baada ya kujiunga na mitandao hiyo ya kijamii

Mpaka kufikia saa 6:00 usiku wa Alhamisi ya Oktoba 1,2015 tayali watu waliokuwa wameshamfuatilia kwenye twitter ni 1,435 na kwenye ukurasa wake wa facebook kulikuwa na likes 10,050 

Pia kiongozi huyo atatumia ukurasa wake wa facebook kujibu maswali kuhusu kanisa la Waadventista Wa Sabato ambapo watu wataweza kumtumia maswali kupitia anuani yake ya barua pepe ambayo ni e-mail:askpastorwilson@adventist.org na atatoa majibu ya maswali matatu kila ijumaa.

Haifahamiki idadi kamili ya Waadventista Wa Sabato waliko kwenye Twitter na Facebook. Ukurasa wa Facebook wa Divisheni ya Kanisa hilo katika eneo la Kusini mwa Amerika unaonekana kufuatiliwa na watu zaidi ya 877,000 japo hakuna anayafahamu kuwa wote ni Waadventista.

Wasifu wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato kwenye Twitter ambao ni  @AdventistChurch,unafuatiliwa na watu  50,300  na kuufanya kuwa unaongoza kwa kuwa na wafuasi wengi miongoni mwa twitter zinazomiliiwa na makanisa .

Viongozi wengine wa dini walioko kwenye twitter ni Papa Francis ambaye anaidadi ya watu Milioni 25 wanaofuatilia akitumia @Pontifex ambayo inatumia lugha 9 kuwasilia na Dalai Lama ambaye anawatu wanaomfulia milioni 11.9