OnlineThursday, June 18, 2015

SERIKALI YA TANZANIA KUJENGA KITUO CHA KUHIFADHIA DATA JIJINI DAR ES SALAAM

Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Prof Makame Mbarawa akihutubia


Balozi wa China nchini Tanzania nchini Lu Youqing

MC wa tukio Isaac Mruma toka TCRA

Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia nchini Tanzania  Prof Patrick Makungu na Mkurugenzi Mtenda wa HUAWEI Zhang Yongquan wakitia saini mkatabaMkurugenzi Mtenda wa HUAWEI Zhang Yongquan akihutubia

Mitambo ya Data ya HUAWEI iliyotolewa

Kituo cha Utunzaji wa Data kitakachojengwa Kijitonyama,jijini Dar es salaam kitakavyonekana baada ya kukamilika
Jumla ya dola milioni 93.77 za kimarekani sawa na takribani shilingi trioni  1.9 za kitanzania zitatumika kujenga mitambo ya kituo cha kuhifadhia data cha Tanzania ikiwa ni mkakati wa serikali ya nchi hiyo  katika kujenga miundo mbinu ya teknolojia ya habari na mawasilino (teknohama) nchini.

Ujenzi wa mitambo hiyo umetiwa saini kwenye mkataba baina ya  Serikali ya Tanzania na Kampuni ya mawasiliano ya HUAWEI leo jijini Dar es salaam ambapo ulishuhudiwa na waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia nchini Tanzania,Profesa Makame Mbarawa,Balozi wa China nchini Lu Youqing na wadau mbalimbali wa teknolojia ya habari na mawasiliano toka serikalini na makampuni mbalimbali.

Waziri Makame Mbarawa amesema  kuwa kituo hicho kitakachojengwa katika eneo la kijitonyama jijini Dar es salaam kitakuwa ni kituo kikubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati ikiwa ni hatua ya tatu baada ya ujenzi wa mkongo wa Taifa na kitakuwa kikitunza data za Serikali,Makampuni ya simu na makampuni mengine binafsi.

Waziri Mbarawa amesema serikali inapaswa kuwekeza katika teknolojia za kisasa ili kuleta maendeleo katika sekta mbalimbali nchini Tanzania.
Friday, June 5, 2015

JE UMEPATA WINDOWS 10 YA BURE

Windows 10 upgrade


Watumiaji wa WINDOWS , je umepata ofa ya WINDOWS 10 ya bure toka kwa Microsoft ?

Jambo hili liko hivi, Microsoft wanatuma ujumbe kwa kompyuta yako kukutaarifa kuwa ufanye uchaguzi kama unataka wakutumie Windows10.

Kama unatumia Windows ambayo ni feki, basi ofa hii sahau.

Na:John Gabriel

UCHINA YAKANA UDUKUZI NCHINI MAREKANI

 

Uchina imetaja kama kukosa kuwajibika ipasavyo kwa Marekani kudai kuwa wadukuzi wa Uchina ndio waliosababisha udukuzi wa taarifa za ofisi za serikali ya Marekani.

Wizara ya mambo ya nje ya Uchina imesema ni vigumu kujua chanzo cha udukuzi huo na kwamba dhana isiyo na ushahidi wowote wa kisayansi haitasaidia.

Shirika la ujasusi la FBI chini Marekani linachunguza ni kwa namna gani wadukuzi wa komputa waliweza kuingilia taarifa hizo binafsi za wafanyakazi wa serikali wapatao milioni nne .

Ofisi ya utumishi ya nchini hiyo inasema karibu watu milioni nne ambao wanafanya kazi au waliwahi kufanya kazi wameathirika na udakuzi huo.
Chanzo:BBC

TAARIFA ZA WAFANYAKAZI ZADUKULIWA MAREKANI

Rais Barak Obama wa Marekani

Serikali ya Marekani imekumbwa na udukuzi wa mtandao wa komputa ambapo taarifa binafsi za mamilioini ya wafanyakazi wa serikali zimeingiliwa.

Ofisi ya utumishi wa nchini inasema takriban watu milioni nne ambao wanafanya kazi au waliwahi kufanya kazi wameathirika na udukuzi huo.

Idara ya Utumishi ya Serikali ya Marekani inayosimamisha huduma za wafanyakazi wa umma nchini huo imefanya uchunguzi wa usalama wa taarifa za wafanyakazi wake wapatao milioni nne.

Idara hiyo inasema wadukuzi hao walingilia taarifa hizo kwa njia ya mtandao tangu mwezi aprili jambo linalofanyiwa uchunguzi na shirika la kijasusi la FBI.

Taarifa zote za udukuzi huo na idadi ya watu waliohusika bado haijafahamika lakini afisa mmoja anasema kila idara ya serikali itakuwa imeathirika kwa kiasi kikubwa.

Mjumbe wa Kamati ya kiintelejensia ya baraza la Seneti imewalaumu wadukuzi kutoka nchini China kwa kuhusika na udukuzi huo.

Hii sio mara ya kwanza kwa taarifa muhimu kama kama hizo kufanyiwa udukuzi.

Mwezi Machi mwaka jana,wadukuzi walijaribu kuwadukua wafanyakazi wa serikalini ambapo pia mwezi Novemba taarifa za wafanyakazi wa wizara ya mambo ya ndani wapatao elfu ishirini zilidakuliwa.
Chanzo:BBC

TANZANIA KUATHIRIKA ZAIDI NA UHALIFU MTANDAO

 
Yusuph Kileo akitoa mada kwenye mkutano huo
Mazungumzo ya awali kabla ya mkutano wa wanausalama mitandao uliokamilika jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini yanaweza kusomeka kwa "KUBOFYA HAPA"  Mkutano ambao uliokua na vuta nikuvute kupata suluhu ya changamoto tulizo nazo za kiusalama mtandao duniani kote zinazoendelea kukua kila kukicha huku ikionekana dhahiri kabisa wahalifu mtandao wanaelekea kuzidi nguvu huku Tanzania ikiorodheshwa kuwa ya sita kwa nchi zinazotegemewa kuathirika zaidi na uhalifu mtandao barani Afrika.

Akitolea ufafanuzi wa takwimu hizi Bwana Vernon Frye, Mkuu wa Usalama mitandao wa kampuni ya Vodacom ya Afrika Kusini, alielezea kuhusiana na uhalifu mpya wa Ransomware ambapo tayari athari zake zimesha onekana Nchini huku akiibua mjadala mzito wa wapi tume jikwaa.
 
Aidha Mjadala mrefu kutoka kwa aliyekua Mkurugenzi wa wakala wa usalama wa Marekani (National Security Agency – NSA) Bwana William Binney pamoja na Raisi na muanzilishi wa kivinjari cha aina ya Tor kinachotumika sana na jumuia ya wana usalama mitandao waliibua changamoto ya ufaragha baina ya watumiaji wa mitandao na namna ya kuendelea kuhakiki kunapatikana uthibiti wa faragha hizi kutotumika vibaya na wahalifu.
 
 
Akiwasilisha mada ya changamoto tulizo zazo barani Afika na nini kifanyike ili kujikwamua katika hali mbaya tuliyo nayo hivi sasa ya wimbi la uhalifu mtandao barani afrika ambapo umeendelea kugharimu bara katika Nyanja za kisiasa, kijamii pamoja na kiuchumi. Yusuph Kileo toka Tanzania alielezea kwa kina mambo ya msingi tunayo takiwa kuyafanyia kazi ili kuhakiki Bara linabaki salama.

Katika mjadala huu ambapo wanausalama mtandao kutoka maeneo mbali mbali ya dunia waliunga mkono alichozungumza kuwa bado kuna kusua sua katika ushirikiano wa pamoja katika kutokomeza uhalifu mtandao huwa wahalifu mtandao kuonekana niwenye ushirikiano ulimkubwa kabisa.
 
Aidha alifafanua kuhusiana na mipango isiyo endelevu ya kukuza vipaji vya wana usalama mtandao wa ndani pamoja na kuwa na program za kukuza uelewa kwa jamii juu ya matumizi salama mitandao ambazo hazionyeshi athari kutokana na uhaba wa maandalizi sahihi na kujua walengwa stahiki.

Makubaliano yamsingi yalikua ni mengi na kwa uchache ni pamoja na kuhakiki kunakua na program endelevu za kuwa kukuza uelewa wa matumizi salama ya mitandao sanjari na kukuza wataalam wa ndani. Pia Ushirikiano baina ya wanausalama si tu katika ngazi ya kitaifa na kibara bali kidunia imeonekana ni muhimu sana. Aidha makampuni kuhakiki yanatumia teknolojia zinazoweza kuendana na hali ya uhalifu hivi sana na kuhakiki wanaziba mianya ya kihalifu kuanzia kwa wafanyakazi wao imeonekana ni jambo muhimu sana.
 
Aidha mkutano huo ulitoa fursa ya washiriki kupata kubadilishana mawazo kwa nyakati tofauti ambapo mtaalamu huyo wa masuala ya usalama katika mitandao alitumia fursa hiyo kuweza kujifunza mengi kutoka kwa mkongwe wa fani hii na aliyeweza kuongoza wakala kubwa ya usalama mitandao ya nchi ya Marekani kama inavyo onekana pichani.
 
 
 

MWELEKEO WA UGAIDI KATIKA MITANDAO YA KIJAMII

Zaidi ya watu 25,000 wamesafiri kueleka Syria na Iraq kujiunga na vikundi vya kigaidi msukumo mkubwa ukitokana na mitandao ya kiijamii huku idadi hiyo ikiongezeka.

"Ujumbe wa hila unaochochea misimamo mikali ambayo hutumwa kupitia mitandao ya kijamii kama vile Twitter, Youtube na mingineyo inavutia na kuhadaa vijana wanaosaka mambo mbadala ya ajabu. 

Kuna takribani akaunti Elfu 50 zinazounga mkono magaidi wa ISIS. Serikali zinajitahidi kutuma ujumbe zaidi wa kubadili ujumbe huo wa chuki. Vijana hawasaki mambo ya msimamo wa kati, wanasaka kile kinacholenga dira zao na kugusa fikra zao na kuleta mabadiliko ya dhati."

Mdau, mitandao ya kijamii ina nguvu lakini sasa inaonekana ni tishio kubwa katika kuchochea ugaidi.Kuna haja ya serikali na vyombo vyake vya usalama kuweka mbinu madhubuti za kuwaepusha vijana na madhara makubwa ya matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii.
Na:Yusufu Mcharia