OnlineWednesday, May 20, 2015

UNESCO WATOA MAFUNZO YA TEKNOHAMA KWA WALIMU WA VYUO VYA UALIMU HAPA NCHINIMkuu Kituo cha Teknohama cha Ushirikiano wa India na Tanzania  (DIT), Dr. Amos Nungu akiwakaribisha wafanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), wakufunzi pamoja na walimu waliofika kwenye mafunzo ya elimu kwa njia ya mtandao.(Picha zote na Geofrey Adroph wa pamoja blog).
Afisa mipango kutoka UNESCO, Bi Faith Shayo akimkaribisha Ofisa anayeshughulikia na masuala ya Elimu Kitaifa wa UNESCO, Tumsifu Mmari (wa kwanza kutoka kushoto) wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya elimu kwa njia ya mtandao kwa walimu wa vyuo vya elimu
Ofisa anayeshughulikia masuala ya Elimu Kitaifa wa UNESCO, Tumsifu Mmari akifungua mafunzo kupitia njia ya mtandao iliyoandaliwa na UNESCO yaliyofanyika jijini Dar.
Bi. Eunice Gachoka kutoka Kenya Institute of Curriculum Development akijitambulisha kwa walimu (hawapo pichani) waliofika kwenye mafunzo ya kupitia mtandao.
Daudi Mbona mkufunzi kutoka chuo cha DIT akiendelea kutoa mafunzo kwa baadhi ya walimu walioudhuria mafunzo ya kupitia njia ya mtandao yaliyofanyika kwenye chuo cha Dar es Salaam Institute of Technology (DIT) hapa jijini Dar.
Godfrey Haongo mkufunzi kutoka Open University nchini Tanzania akitoa elimu ya njia ya mtandao.
Baadhi ya walimu wanaoshiriki mafunzo hayo. 
 Na Geofrey Adroph, Pamoja blog


 UNESCO imeaandaa mafunzo ya uboreshaji wa elimu kwa walimu hususani katika somo la Teknohama kwa vyuo mbalimbali vya hapa nchini vinavyotoa elimu ya ualimu.

 Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania yamefanyika katika chuo cha Dar es Salaam Institute of Technology (DIT) ili kuweza kuwapa fursa hiyo waalimu wa vyuo mbalimbali katika ufundishaji na uelimishaji namna ya matumizi ya Tehama. 

  Hii inatokana na baada ya mkutano wa viongozi wa vyuo mbalimbali pamoja na wadau wa elimu wa hapa nchini Tanzania hivyo kuona kama kuna mapungufu katika masuala la uelewa na matumizi ya Tehama hasa katika vyuo hivyo.
  
 Baada ya kuona kuna mapungufu hayo UNESCO waliamua kuanzisha mradi uitwao UNESCO-China Funds in Trust Project (CFIT) wakishirikiana na vyuo vya elimu hapa nchini Tanzania waliamua kuanzisha mradi huo kwa malengo makuu matatu ambayo ni kuboresha elimu kwa walimu wa vyuo vya ualimu, kuweka mafunzo ya walimu wanapofundisha katika Tehama ili kuendana na mabadiliko ya teknolojia pamoja na kuwanunulia vifaa vya Teknohama ambavyo vitasaidia katika kufundishia na kujifunzia, Afisa mipango kutoka UNESCO, Bi Faith Shayo alivitaja vifaa hivyo kwa kuviorodhesha kuwa ni pamoja na kompyuta, Projecta, na Sola ili kuhakikisha hakuna tatizo la umeme katika ufundishaji wa masomo hayo .

  Kupitia mradi huo wa (CFIT), UNESCO imeandaa mafunzo ya siku tano kwa walimu wa vyuo vya ualimu kutoka vyuo mbalimbali vya Elimu hapa nchini Tanzania ili kuongeza ujuzi na ufanisi katika ukuzaji wa Teknohama hasa kupitia kwenye njia ya mtandao na pia kuendana na wakati kutokana na mabadiliko pamoja na ukuaji wa matumizi ya Teknolojia Mafunzo haya yaliyoandaliwa na UNESCO yanafanyika katika chuo cha Dar es Salaam Institute of Technology (DIT) kwa ajili ya kuwapa elimu kwa baadhi ya walimu wa vyuo ili kupata uelewa zaidi juu ya Tehama. 

 Wakufunzi wa mafunzo hayo ni Daudi Mboma ambaye ni Mkuu wa idara ya maendeleo ya biashara kutoka (DIT) na Godfrey Haongo kutoka Chuo Kikuu Huria cha Tanzania ambao wanajukumu la kuwafundisha walimu mbalimbali kutoka vyuo tofauti hapa . 

 Waalimu tisa kutoka chuo cha ualimu Tabora, waalimu tisa kutoka chuo cha ualimu Monduli , walimu wanne kutoka chuo cha ualimu Morogoro, mmoja kutoka Shule direct, wawili kutoka Chuo kikuu cha Nelson Mandela, mmoja kutoka Ngorongoro Waso District, pia kuna baadhi ya watakao pata mafunzo hayo wanatokea Wizara ya elimu ambao wanafanya kazi kwa ushirikiano na UNESCO ili kuweza kufikia malengo ya mradi huo kwa vyuo vya elimu hapa nchini.

  Kutokana na kuwa na uelewa mdogo wa masuala ya Teknohama UNESCO wamejipanga kuweza kupambana na kutoa mafunzo ya kiteknolojia ili kuweza kuboresha matumizi na upatikanaji wa huduma za kiteknohama katika taifa la Tanzania kwa kuanzisha mradi huo wa kutoa mafunzo kwa walimu nao walimu waweze kwenda kuutumia ujuzi huo katika ufundishaji kwenye vyuo wanavyofundisha ilikuweza kuwapa upeo mkubwa wanafunzi wa ualimu ambao ndio watakao kuwa kipaumbele katika kufanya nchi iwe katika mfumo mzuri wa Tehama.

Monday, May 11, 2015

VIDEO:JINSI YA KUITUMIA SIMU YAKO YA KISASA AMA TABITI KUWA KAMERA YA ULINZI

Saturday, May 9, 2015

WAADVENTISTA WA SABATO NCHINI TANZANIA WATAKIWA KUTUMIA TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO

Gideon Msambwa akihutubia kanisani Kirumba,Mwanza

Waumini wakimsikiliza Gideon Msambwa

Mkurugenzi wa mawasiliano wa Unioni Konferensi ya Kaskazini  mwa Tanzania ya Kanisa la Waadventista Wa Sabato Gideon Msambwa ametoa ushauri kwa washiriki kutumia teknolojia ya habari na mawasilino ili kuleta maendeleo ya kanisa hilo nchini.

Akizungumza jana  Mei 9 mwaka huu jijini Mwanza katika Kanisa la Waadventista wa Sabato Kirumba,Msambwa amesema Mataifa ya Asia na Kusini mwa Bara la Amerika yamepiga hatua kubwa katika Teknolojia ya Habari na Mawasiliano,hadi kufikia hatua ya kumiliki viwanda.

Akitoa mfano, amesema Kanisa la Waadventista wa Sabato Korea Kusini linamiliki viwanda vidogo 104,000 wakati Tanzania bado kanisa hili linamiliki kiwanda kimoja cha Uchapaji kilichopo mjini Morogoro.


Amesema pia kwamba, Korea Kusini kuna vyuo vikuu vitano vya Kimataifa,wakati hapa nchini Waadventista wa Sabato wanamiliki Chuo kikuu kimoja,University of Arusha.


Korea Kusini kanisa hili humikili kiwanda bora cha uchapaji,wakati nchini Brazil kanisa hili washiriki wake wamepiga hatua kubwa katika medani ya elimu na teknolojia.


Mkuu huyu wa Mawasiliano katika Union Konferensi ya Kaskazini mwa Tanzania,amesema asilimia 60 ya wabunge Brazil ni Waadventista wa Sabato,huku washiriki wa kanisa wameunganishwa katika Mfumo wa kiteknolojia wa kutunza kumbukumbu uitwao,Adventist Church Manegement System(ACMS),ambamo kumbukumbu zote za washiriki na wachungaji hutunzwa.


Kufuatia hali hiyo,Tanzania na Ghana zimechaguliwa na Konferensi Kuu(GC) kuandaa mfumo huu wa kutunza kumbukumbu.


Hadi sasa, Union 38 hapa duniani za kanisa hilo kumbukumbu zake zimehifadhiwa katika Mfumo huu wa ACMS.Jumla ya washiriki waliobatizwa wa Kanisa 7,500,313 kumbukumbu zao zinahifadhiwa katika mfumo huu duniani,miongoni mwa hawa 1,679 ni wa makanisa 1,735 ya Unioni ya Kaskazini mwa Tanzania.


Unioni ya Kaskazini mwa Tanzania(NTUC) ina jumla ya washiriki waliobatizwa 354,456 wakati washiriki wengi kumbukumbu zao zikiwa hazijaingizwa katika mfumo huu mahsus wa kumbukumbu.


Kufuatia hali hiyo,Idara ya Mawasiliano ya Unioni hii imewataka wachungaji na washiriki kuhakikisha kuanzia sasa hadi Disemba 2016 asilimia 50 ya kumbukumbu zote za washiriki ziwe zimeingizwa katika mfumo huu.


PROGRAM TUMISHI YA M-PESA YAWA MIONGONI MWA PROGRAM TUMISHI ZINAZOWAWEKA MAMILIONI YA WATU MTANDAONI KWA KUTUMIA SIMU

 Five Mobile Apps Bringing The Next Billion People Online

 Mwaka  2013, Mwenyekiti Mtendaji wa Google Eric Schmidt alikisia kuwa duniani kote watu watakuwa kwenye mtandao mwishoni mwa karne.

Kuna progam tumishi nyingi ambazo zimetengezwa na zinatengezwa zikijaribu kuwaweka watu karibu kwenye mitandao .
Ripoti iliyolewa hivi karibuni inaonesha kuwa kuna baadhi ya program tumishi ambazo zitasaidia kwa kiwango kikubwa kuwaweka mtandaoni mamilioni ya watu duniani  miongoni mwa program hizo maalufu ambazo zinaonekana kuongoza kupitia simu za mikononi ni;

1. M-Pesa
Hii ni Program tumishi kwa ajili ya malipo kupitia simu za mkononi ambayo inatumika barani Afrika huduma iliyoanzishwa mwaka 2007 na kampuni ya Safaricom ya nchini Kenya iliyomiongoni mwa makampuni ya  Vodafone,Mtumiaji anaweza tuma ama kupokea fedha kupitia ujumbe mfupi wa maneno,kulipa bili na kununua muda wa maongezi.Katika maeneo ambapo watu wanapata huduma chache za kibenki ama hakuna huduma hizo M-Pesa imekuwa ikipata umaarufu ambapo kwa sasa inaonesha kufikisha kiasi cha watumiaji milioni 18 wa huduma hiyo.


2. SoukTel
Ikiwa inatumika Mashariki ya Mbali, SoukTel ina program tumishi mbalimbali zinazowasaidia watu kupata taarifa kuhusu kazi na huduma za kijamii.Inajuikana hasa kwa kuhusianisha katika kutafuta kazi na inawaunganisha watu mbalimbali kupitia ujumbe mfupi wa maneno toka Jordan,Rwanda,Tunisia na nchi mbalimbali.Hivi karibuni SoukTel iliungana na Facebook na kuanzisha huduma ya elimu ya uchumi nchini Colombia.


3. Esoko
Mara nyingi huelezwa kuwa ni Facebook kwa ajili ya wakulima Esoko inawaunganisha wakulima na mashirika yasiyo ya kiserikali,makampuni ya biashara na wakala wa serikali .Soko ni neno la kiswahili linalotokana na sokoni na E ikisimama badala ya vifaa vya umeme.

Utumaji wa ujumbe mfupi wa maneno kwa kuhusianisha tovuti ambapo hutuma taarifa kuhusu hali ya hewa,taarifa za bei na matangazo.

4. Frogtek
Kwa kutumia program za simu za kisasa na tabiti, Frogtek inasaidia wafanya biashara wadogo hasa katika familia ndogo maarufu  mom-and-pop katika nchi za bara za Amerika ya Kusini na baadhi ya nchi zinazoendelea ambapo huwawezesha wafanyabiashara hao kufahamu bidhaa walizonazo na mauzo yaliyofanyika 


5. Ver Se’ Innovation
Imetengenezwa huko Bangalore, India,ni program tumishi ambayo ni maalum kwa taarifa na huduma za ndani ya India ambayo husaidia kutoa taarifa za kazi,umiliki wa vitu mbalimbali na matangazo ya masoko huku ikiwa na huduma ya malipo na manunuzi kwa njia ya mtandao.
SERIKALI YA TANZANIA YAWATAKA WANANCHI KUTOA MAONI YA KUBORESHA SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAO 2015


 

Serikali ya Tanzania imewataka wananchi kutoa maoni yatakayoiboresha sheria ya makosa ya mitandao ya mwaka 2015 iliyosainiwa hivi karibuni na Rais Jakaya Kikwete ili yasaidie kuiboresha.
Imesema licha ya sheria hiyo kusainiwa na Rais, bado kuna umuhimu wa kuiboresha katika baadhi ya vipengele vyenye upungufu.

Kauli hiyo imetolewa Mei 8 mwaka huu jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa (Pichani) katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika ofisini kwake.

Mkutano huo uliandaliwa maalumu kwa ajili ya kuufahamisha umma kuhusu kusainiwa kwa sheria hiyo na rais wa Tanzania na kuelezea umuhimu wake, huku pia waziri huyo akiitumia fursa hiyo kukaribisha maoni ya wadau mbalimbali kwa ajili ya kuiboresha.


“Tunaomba wananchi tuipokee sheria hii kwa sababu ni nzuri na itasaidia sana kuwalinda, lakini pia kama kuna kifungu chochote ambacho kitaonekana kuwa na upungufu leteni ushauri au maoni wizarani, tutayatafakari na tutayafanyia kazi,” alisema Mbarawa.

Waziri Mbarawa amesema Tanzania si nchi ya kwanza kupitisha sheria ya aina hiyo kwa sababu ya uwepo wa maendeleo ya teknolojia ya mawasiliano kulikosababisha kuongezeka kwa uhalifu wa mitandao.


  Profesa Mbarawa amesema nchi za Uingereza, India, Malaysia, Uganda, Korea Kusini, Singapore, Mauritius, Afrika Kusini, Marekani na nyinginezo tayari zina sheria ya aina hii na inasaidia kuwapa wananchi haki wanapofanyiwa uhalifu wa mitandaoni.

Sheria ya Makosa ya Mitandao mwaka 2015 ni moja ya sheria zinazokosolewa  na wadau wa habari pamoja na makundi mbalimbali ya kijamii, kwa madai kuwa inalenga kubana uhuru wa vyombo vya habari pamoja na kubinya uwanja mpana wa ukusanyaji na utoaji habari kwa waandishi wa habari.

Saturday, May 2, 2015

TAHADHARI KWA WANAOANGALIA TOVUTI ZA PICHA ZA NGONO KATIKA SIMU ZAO


Watafiti toka kampuni ya utafiti ya  Zscalar  wamegundua kuwa,tovuti za kichina zenye picha za ngono zimekuwa zikisambaza virusi ambavyo vinasababisha simu za mikononi kushambuliwa na virusi vya komputa viitwavyo malware.
Utakapotembelea tovuti hizo na ukajaribu kuangalia video,tovuti itakuomba upakue sehemu ya program ya komputa ambayo kiuhalisia ni kirusi kiingine kiitwacho trojan.

Kirusi hicho cha Trojan kinajishajilisha chenyewe kwenye simu yako na kuifanya simu yako kuwa na uwezo wa kupokea matangazo yanayohusisha  ujumbe mfupi wa maneno (sms) ulioko kwenye simu yako.Jambo ambalo litasaidia wahalifu wa mtandao kudukua taarifa zako za kibenki kwenye simu iliyo na kirusi hicho kiurahisi.


MWANAFUNZI AFUNGWA JELA MIAKA MINNE KWA KOSA LA KUDUKUA KOMPUTA ZA CHUO KIKUUMwanafunzi mwenye umri wa miaka 25 ambaye alidukua komputa za Chuo Kikuu cha Birmingham na kuongeza alama za mtihani amefungwa jela miaka 4.

Imran Uddin, ambaye alikuwa anasoma mwaka wa mwisho fani ya sayansi katika chuo hicho aliongeza alama za mtihani toka asilimia 57 hadi 73 kwa kuiba neno la siri la mfanyakazi kwa kutumia keybord inayodukua yenye uwezo kudukua komputa aliyoinunua baada ya kuitafuta kupitia mtandao wa ebay.Kwa mujibu wa mahakama inaelezwa kuwa Uddin alipachika nyuma ya komputa  kifaa kinachoweza kuingia kwenye program ya komputa bila mhusika kutambua.Tukio hilo lilitokea Oktoba 7 mwaka jana ambapo kifaa hicho kilikuwa kikichukua taarifa ya kila kilichofanywa na mtumiaji wa komputa hiyo  na baadaye ilionekana vifaa kama hivyo vilikuwa vimewekwa katika komputa tofautikati chuoni hapo.

Friday, May 1, 2015

MFUMO WA UNUNUZI WA UMEME KUPITIA SIMU ZA MIKONONI WAVUNJWA

Baadhi ya wakazi wa jijini Dar es salaam wakiwa wamepanga foleni ili kununua umeme jana

Huduma ya manunuzi ya umeme kwa njia ya miamala ya simu za mkononi nchini Tanzania imeanza kuwa kero kuanzia jana Aprili 30 mwaka huu baada ya kile kinachoelezwa kuwa ni kuvunjika kwa mkataba kati ya Shirika la Umeme Tanzania-Tanesco na mmoja wa watoa huduma hiyo ya ununuzi wa umeme yaani kampuni ya Selcom ambapo mteja hupatiwa namba ambazo huziingiza kwenye mita ya luku.

Katika mfumo huo mteja hununua umeme kupitia simu ya mkononi kupitia Mpesa, Tigo Pesa na Airtel jambo ambalo kuanzia jana haliwezekani kwa sasa ambapo kampuni ya Tigo ilianza kuwatumia ujumbe wateja wake kuwa imesitisha huduma hiyo kutokana na matatizo na wakala.

Hali ilivyokuwa:
  • Manunuzi yote ya luku yalikuwa yakifanyika kupitia mitambo ya makampuni mawili, Maxcom na Selcom.
  • Makampuni haya ndiyo yanayowapa wengine kama vile mitandao ya simu na mabenki uwezo wa kununua na kulipia huduma ya umeme -Luku
  • Hivyo mara nyingi pale ulipokuwa unapata shida kununua umeme inakuwa pale ambapo mfumo wa malipo unaotegemea mitambo ya moja ya hizi kampuni mbili unakuwa na hitilafu.
Tanesco kupitia amri ya WAZIRI wa Nishati na Madini, George Simbachawene,  na ushauri wa TRA wamevunja mkataba wa uwakala na Kampuni ya Selcom. Sababu kubwa zilizotolewa ni kutokana na mitambo yake ya kuuza umeme kwa njia hii kuwa na matatizo ikiwemo matatizo ya kisheria katika kulipa kodi.

Inasemekana kero nyingi za ukosekaji wa huduma ya manunuzi ya umeme wa LUKU ambayo imekuwa ikitokea hivi karibuni imekuwa ni kutokana na mitambo ya kampuni hii kusumbua.

Kwa kuwa kabla ya hili kutokea makampuni ya simu na baadhi ya mabenki yalikuwa yanatoa huduma hiyo ya ununuaji wa umeme kupitia mitambo ya Selcom kwa sasa utaendelea kukosa huduma hiyo.

Kwa sasa wanunuzi wa umeme kwa njia ya luku wataendelea kupata huduma hiyo kupitia vituo vya mauzo ya Luku vya Tanesco au sehemu inayouza umeme kupitia huduma ya MaxMalipo.

 credit:www.teknokona.com