OnlineTuesday, April 21, 2015

PROGRAM TUMISHI ZA SIMU ZINAZOWAWEKA KARIBU WANANDOA


 http://wp.production.patheos.com/blogs/danpeterson/files/2014/10/black-couple-hugging.jpg
Mabadiliko ya teknolojia ya mawasiliano yanayotokea duniani yamekuwa yakileta athali chanya na hasi ndani ya jamii hasa katika maswala ya mawasiliano.
Wavumbuzi na wataalamu wa program tumishi duniani nao hawako nyuma katika kubuni programu ambazo zitawafanya wachumba ama wanandoa wanaotumia simu za kisasa na tabiti kuwa karibu zaidi katika masuala ya mawasiliano.
Kwa sasa kuna program tumishi nyingi ambazo ni maalum wa wapenzi ama wanandoa japo kuwa kuna zile ambazo zinaleta tija zaidi ya nyinginezo.
Couple
Kanuni iliyoko katika program tumishi ya Couple ni kwamba inawawezesha watu wawili kuwa na wigo wa mawasilino ya mahusiano yenye  faragha kwa kubadilishana picha,video,ama ujumbe wa sauti
Hii ni program tumishi ina huduma ya kutuma ujumbe wa papo kwa papo kama ilivyo katika mtandao wa kijamii wa WhatsApp,picha inaweza kutumwa ikiwa imewekwa katika mpangilio wa kutoweka baada ya muda fulani pia ina huduma ya kukupatia taarifa ya mahali pa faragha  ambapo mnaweza kwenda kwa ajili ya chakula ama maongezi ya wachumba ama wanandoa,ikiambatanisha na kalenda.
Mpaka sasa inatumiwa na wanandoa zaidi ya milioni mbili duniani ni moja ya program tumishi ambayo inaonekana kuwafaa wanandoa katika mawasiliano binafsi ya faragha.

Couple Tracker

Imekuwa ni jambo la kuumiza kwa baadhi ya watu walioko kwenye mahusiano.Jambo hili limekuwa likileta lawama na kushutumiana katika suala kukosa uaminifu.

Couple Tracker ni program tumishi iliyokusudia kutatua tatizo la watu kutokuwa waaminifu  kwenye mahusiano na imekusudia kuwa na mkakati wa kusaidia kuboresha uaminishi kwenye mahusiano ya wachumba ama wenzi wa maisha.

Kinachofanywa na program hii tumishi ni kumwezesha mwanandoa kuona simu zilizopigwa,kupokelewa,ujumbe mfupi wa maneno,anachofanya mwanandoa mwenzake kwenye mitandao ya kijamii ya  Whatsapp, Facebook  na uwezo kutambua mahali simu ya mwanandoa ama mchumba mwenzako ilipo,japo kuwa ina sehemu fulani ya faragha hata hivyo mawasiliano yote ya masaa 24 katika siku saba yanaweza kuoneshwa kwa kupitia program hii.

Hata hivyo ni lazima uhakikishe kuwa kuna makubaliano rasmi ya wahusika wawili  kuitumia kwa sababu ya sheria zinazozuia udukuzi wa mawasiliano.

Our Groceries


Watalaamu wa mahusiano wanaeleza kuwa maisha ya ndoa baada ya fungate huwa yanachangamoto zake hasa katika masuala ya kipato katika matumizi mbalimbali ya fedha za kujikimu kwa wanandoa.
Kila mmoja analojukumu la kuhakikisha masuala ya manunuzi ama gharama za matumizi ya nyumbani mfano malipo ya umeme,maji ,malipo na manunuzi ya vifaa mbalimbali vya familia.
Our Groceries ni program tumishi ambayo inajaribu kutoa suruhisho la kutatua upangaji wa bajeti kwa wanandoa  na hivyo kuepusha manunuzi ambayo unaweza yafanya wakati ambapo mwenzi wako ameshayafanya kwa kuwa inakupa taarifa ya kile mwenzako alicho kinunua kabla.
Kwa kutumia progam hii unaweza kutayarisha orodha ya mahitaji unayopanga kununua ama kuyafanyia malipo na ukamshirikisha mwenzi wako kuona orodha hiyo  na utakapofanya malipo ama kununua chochote basi itatuma taarifa kwa kifaa cha mawasiliano cha mwenzi wako na kama unahitaji kutoa taarifa  anunue bidhaa yoyote unaweza fanya hivyo pia.

Avocado

Kama ilivyo program tumishi ya Couple, Avocado inawezesha kuwapatia wanandoa mawasiliano ya faragha na kuwaunganisha katika mawasiliano muda wote.
Unaweza kumtumia mwenzi wako ujumbe mfupi wa maneno,video,sauti na imewekewa kalenda ambayo hukumubusha matukio muhimu ya kuyakumbuka ikiwemo siku ya kuzaliwa,siku ya kufunga ndoa na mambo mengine muhimu kwa wanandoa.

Kwa wale waliona mahusiano yanayotenganishwa na umbali inasaidia kukufanya uhisi kuwa karibu na umpendaye,pia inawezesha kutoa taarifa kwa mwenzi kuwa karibu betri ya kifaa cha mawasiliano itazima,programu hii pia inamwezesha mtumiaji kuona ujumbe,picha na taarifa zingine hata kama haujaunganishwa na upande mwingine wa mwenzi wako.
Inawezesha pia kuficha taarifa za mtumiaji ili mtu mwingine asizione ama kuzipata.

Hizi ni baadhi tu ya program tumishi nyingi ambazo zinaweza kusaidia kuwaweka karibu zaidi wanandoa na kuboresha mahusiano yao siku baada ya siku ..Friday, April 17, 2015

WAHALIFU WATENGENEZA KIRUSI KINACHOWEZA KUDUKUA SIMU YA MKONONI IKIWA IMEZIMWA Malware That Can Spy On Your ‘Powered Down’ Phone

Watu wengi wameshaona filamu ambazo wahalifu  wakidukua simu  za mikononi hata kama zimezimwa.

Kama ilivyozoeleka kuwa watu wengi hufikiri mambo hayo ni ya kufikirika.

Hata hivyo hivi karibuni kampuni ya AVG inayojihusisha na masuala ya usalama katika simu za mikononi na imegundua virusi aina ya  malware kilichopewa jina la ‘PowerOffHijack,’ambavyo vinauwezo wa kuingilia mfumo wa kuzima simu na kuifanya simu ya mkononi iendelee kupatikana japo imezimwa..

Kirusi huyo mara ya kwanza ameonekana nchini China na kusambaa katika program tumishi za uchina na simu nyingi zimeshambuliwa na kirusi huyo hasa zilizotengenezwa kwa program endeshi za Android zenye zaidi ya toleo namba 5

Kirusi hicho kikiingia kwa simu ya mkononi simu itatoa ujumbe kuwa imezimwa na malware itawe kupiga simu,kupiga picha na kufanya mambo mbalimbali bila mwenye simu kutambua.

Wednesday, April 8, 2015

UTAFITI:SIMU ZINACHANGIA UMASKINI NA MIGOGORO KATIKA MAHUSIANO


 
Wataalamu wa Saikolojia kutoka Chuo Kikuu cha Pennsylvania na Chuo Kikuu cha Vijana cha Bringman nchini Marekani wamebaini kuwa matumizi ya simu ni chanzo cha kutofurahia maisha na kuongeza msongo.
Utafiti uliofanywa na wataalamu hao chini ya usimamizi wa Brandon McDaniel,Mkufunzi kutoka Chuo Kikuu cha Pennsylvania,ulibainisha kuwa watu wengi wanaongeza umaskini wa kujitakia kwa kutumia muda mwingi kwenye simu.
Wanazungumzia maisha ya watu,mafanikio yao,kushindwa kwao badala ya kuangalia vitu vitakavyowaingia fedha zaidi,inaeleza sehemu ya utafiti huo.
Utafiti huo ulibainisha kuwa mbali na umaskini wa kujitakia,matumizi ya simu kupita kiasi huchangia kwa asilimia 75 ndoa kuvunjika pia hatari ya kupata msongo wa mawazo.
Utafiti huo uliohusisha watu wazima 867 wenye umri wa miaka 30 hadi 45,ulibainisha kuwa kama wasingekuwa na simu,robo tatu ya watu hao wangekuwa wamefanya mambo mengi kuboresha maisha yao ikiwemo utendaji bora wa kazi.
Majibu ya utafiti huo yalionesha kuwa wanandoa wengi wangepata muda wa kujadili namna ya kumaliza tofauti zao,kufikia mafaniki,kutimiza malengo hata kuboresha penzi kama wasingetumia simu.
Takwimu za Mamlaka ya Mawasiliano nchini Tanzania (TCRA) zinaonesha kuwa mwaka 2014 kulikuwa na laini za simu za mkononi zipatazo 31,862,656,ikilinganishwa na laini 2,963,737 mwaka 2005,watumiaji wa intaneti wameongezeka hadi kufikia 11,000,000 Desemba mwaka 2014 kutoka 3,563 waliokuwepo mwaka 2008
Chanzo:Gazeti la Mwananchi

Thursday, April 2, 2015

DAR ES SALAAM:MATANGAZO YA TV YA ANALOJIA MWISHO JUNI 17,2015 NCHINIMamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) na Shirika la umoja wa mataifa la Mawasiliano ya simu ulimwenguni ITU kwa  pamoja wameridhia makubaliano ya kusitisha Mfumo wa utangazaji wa televisheni unaotumia teknolojia ya analojia  katika miundombinu ya minara ifikapo juni 17,2015 na kuanza kutumia mfumo wa utangazaji wa kidijitali pekee.


Akizungumza na waandishi wa habari  hii leo jijini Dar es salaam Meneja mawasiliano wa TCRA Innocent  Mungy  amesema  makubaliano hayo ya jumuiya za ushirikiano wanchi mbalimbali zimechukua hatua za pamoja kuhakikisha uhamaji kutoka mfumo wa utangazaji wa anolojia kwenda dijitali unafanikiwa.


Mungy amesema Tanzania imekuwa nchi ya kwanza kutekeleza maazimio ya nchi wanachama na uzimaji wa mitambo ya televisheni inayotumia teknolojia ya analojia  Tanzania Bara ilianza kufanyika desemba  31,2012 .

Amekuwa Mamlaka kwa kushirikiana na Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Wizara ya Habari Utamaduni na michezo na  wadau wengine itaendelea kutoa elimu kwa umma ili kuhamasisha uhamaji pamoja na kuwaelewesha watumiaji haki zao za msingi.  

KAMATI YAPENDEKEZA SERIKALI KUONGEZA ADHABU KWA WATAKAOTUMA TAARIFA ZA UONGO KWENYE MITANDAO

Kamati ya kudumu ya Bunge ya miundombinu imependekeza kwa serikali iongeze adhabu ya faini kutoka shilingi milioni tatu na kifungo kisichopungua miezi sita na kuwa faini ya shilingi milioni tano na kifungo kisichopungua miezi sita kwa wale wote watakaotuma katika mtandao taarifa za uongo.

Aidha kamati hiyo ilipendekeza katika adhabu kwa watu wanaonyanyasa wenzao kupitia mtandaoni adhabu yao iongezwe kutoka kifungo cha cha mwaka mmoja na kuwa kifungo cha miaka mitano.

Awali akiwasilisha maelezo ya muswada huo,Waziri wa Mawasilino,Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa alisema kutokana na kukua kwa matumizi ya teknolojia ya Habari na Mawasiliano kumesababisha kuwepo kwa changamoto mbalimbali ikiwemo kuibuka kwa makosa ya mtandao.

Alitaja makosa ya mtandao yaliyokithiri kwa sasa kuwa ni makosa dhidi ya faragha,usalamana upatikanaji wa taarifa za kompyuta na mifumo ya kompyuta,makosa yanayohusu maudhui,makosa dhidi ya mifumo ya kompyuta na makosa ya kawaida yanayofanywa kwa kutumia mitandao.

Profesa Mbarawa alisema kuwa takwimu kutoka jeshi la polisi zinaonesha kuwa makosa ya uhalifu wa mtandao yaliyoripotiwa na kuchunguzwa kati ya mwaka 2012 hadi Agosti mwaka jana ni 400.

Alisema katika kipindi cha mwaka 2000 hadi mwaka 2013,makosa ya uhalifu wa mitandao yalisababisha hasara ya zaidi ya shilingi bilioni 9.8 kwenye taasisi za fedha.