OnlineTuesday, February 24, 2015

GOOGLE KUWABANA BLOGGER WANAOWEKA PICHA NA VIDEO ZA NGONO KUANZIA MACHI 23,2015

 Image result for google

Kampuni ya mtandao ya Google imetoa tangazo kwa watengenezaji wa blog  kuwa kuanzia Machi  23, 2015, hawataruhusiwa kuweka ama kutangaza picha na  video za ngono ama zenye mwelekeo huo katika blog wanazozimiliki.

Taarifa hiyo ambayo imetolewa juma hili kwa blogger inaeleza kuwa picha na video zenye mwelekeo huo hazitaruhusiwa kuonekana kama ilivyosasa kuanzia siku hiyo.

Google imeeleza mabadiliko haya ya sera zake yanawataka wote walio kinyume na sera hiyo kuhakikisha wanafanya mabadiliko kwenye aina ya habari wanazozichapicha kwenye blog zao kabla ya muda huo ambapo wanatakiwa kuondoa picha na video za ngono ama kuzifanya blog binafsi na wasipofanya hivyo google watafanya mabadiliko ama kuiondoa blog hiyo.Saturday, February 21, 2015

UINGEREZA NA MAREKANI ZINADUKUA SIMU YAKO

 

Majasusi wa Uingereza na Marekani walikiuka sheria na kudakua kampuni inayotengeneza kifaa kinachotumika kwa simu za mkononi yaani ''Sim Card''Tovuti moja ya habari za teknolojia imeripoti huko Marekani.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo Majasusi hao waliiba mfumo na data inayowaruhusu kusikiza mawasiliano mbali na kujua alipo mmiliki wa simu hiyo lengwa.

Habari hiyo ambayo chanzo chake inasemekana kuwa ni aliyekuwa mfanyikazi wa shirika la ujasusi la Marekani CIA, Edward Snowden
inaziwezesha mashirika hayo mawili ya kijasusi kudukua mamilioni ya simu za mkononi kote duniani.

Kampuni hiyo lengwa Gemalto imesema kuwa imeshtuliwa na madai hayo na kuwa inayachunguza kwa kina.

Kampuni hiyo inahudumia mataifa 85 kupitia mashirika 40.
Aidha kampuni hiyo inahudumia makampuni 450 kote duniani.

Habari hiyo inaeleza kuwa wateja wa kampuni ya simu ya AT&T, T-Mobile, Verizon, Sprint na kampuni zingine 450 kote duniani zimeathirika.

Taarifa hiyo inasema kuwa udukuzi huo ulifanyika tangu mwaka wa 2010.

Mwandishi wa BBC aliyeko mjini Washington Marekani Naomi Grimley anasema wizi huo umewawezesha majasusi wa Marekani na Uingereza
kudukua simu za wateja mataifa ya kigeni na hata kunakili jumbe zinazotumwa kutoka kwa simu hizo bila ya kuomba ruhusa kutoka kwa serikali ama makampuni ya simu.
Chanzo:BBC

Friday, February 20, 2015

MAMILIONI YA DOLA YAIBIWA KATIKA MABENKI KUPITIA WIZI MTANDAO

 http://2.bp.blogspot.com/-I1cf5hw6HFs/VOR0A0M0fNI/AAAAAAAABRw/gTcPxKp2gLw/s1600/ATM-Theft.jpg
Baada ya kikao kilichofanyika juma liliyopita katika Chuo Kikuu cha Stafford ambapo Rais Obama wa Marekani alikutana na wafanya biashara, Wanasheria na wasimamizi washeria kujadili hali ya mtikisiko wa maswala ya usalama mitandao, Inadhihirisha wazi bado kuna safari ndefu kukabiliana na wimbi hili la uhalifu mtandao duniani kote.

Hii ni kutokana na ukweli kwamba Tishio la uhalifu mtandao na utayari wa kukabiliana nao bado kuna kutowiana ipasavyo ingawa jitihada bado ni kubwa kuweza kukabiliana na uhalifu huu unaokua kwa kasi ya pekee duniani kote.

Wakati haya yakijiri na mikakati zaidi ikiendelea ya kukabiliana na wimbi kubwa la uhalifu mtandao hivi sasa makampuni yanayojihusisha maswala ya fedha yameonekana yakiathirika zaidi na uhalifu mtandao – Hii ni kwamujibu ya ripoti maalum iliyotolewa na kampuni ya Kaspersky Lab.

Taarifa inaeleza kwamba genge la wahalifu mtandao limefanikiwa kuiba Mamilioni ya Dola za kimarekani kutoka kwenye akaunti za wateja wa mabenki 100 katika mataifa 30 kati ya mwaka 2014 na 2015.

Ripoti hiyo inaelezea mbinu mpya za wahalifu mtandao wanazotumia kudukua nambari za akaunti za wateja za siri kabla ya kuingia na kuiba pesa.

Kaspersky imesema kuwa wizi huo ulianza mwaka wa 2013 na bado unaendelea hata leo kwani mabenki yote yalioathirika hayana uwezo wa kuwazuia wezi hao.

Hadi kufikia sasa ripoti hiyo inadai kuwa takriban dola bilioni moja zimeporwa kutoka kwenye akaunti za wateza.

Genge hilo la wezi, lililoanzia shughuili yake nchini Urusi, Ukraine na pia Uchina ndilo linalolaumiwa kwa wizi huo.

Kampuni hiyo ya Kaspersky inasema inafanya juhudi za kuzima wizi huo kwa ushirikiano na polisi wa kimataifa Interpol na polisi wa bara ulya Europol.
 
Kwa mujibu wa ripoti hiyo mabenki katika mataifa 30 yakiwemo, Russia, Marekani , Ujerumani , Uchina, Ukraine na Canada yameathirika pakubwa.

Kamanda wa kikosi cha polisi wa kimataifa Interpol bwana Sanjay Virmani, amesema kuwa wezi wataendelea kutumia upungufu wa miundo msingi katika sekta ya uchumi wa mataifa husika hadi pale kutaibuka umoja wa kuzuia mapengo.

Kaspersky hata hivyo inasema kuwa genge hilo linalenga mabenki bila ya kuwaibia watu binafsi.

genge hilo kwa jina Carbanak, linatumia mbinu ya kuambukiza virusi kwenye mashine za benki ikiwemo kamera za CCTV ilikunakili kila kitu kinachoandakiwa kwenye kompyuta.

Kutokana na uweledi wao genge hilo lilituma pesa kwenye account zao huku wengine wakiamrisha mmitambo ya kutoa pesa ATM kumimina pesa bila kikomo.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo kila tukio la wizi lilihusisha takriban dola milioni kumi.

Kwa Tanzania Hali inaweza kubadilika kabisa siku za usoni kwani tayari mipango na mikakati ya dhati ya kukabiliana na uhalifu huu wa kuibia watu pesa zao kupitia ATM inaendelea kwa kasi na hatima ya kupata muarobaini stahiki unategemewa kutatua hali husika.
Na:Yusuph Kileo

 

Friday, February 13, 2015

WANATEKNOHAMA WA KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO WATAKIWA KUTUMIA USALAMA MTANDAO NA PROGRAM TUMISHI KATIKA UTUME


Baadhi ya Wataalamu wa Teknohama wa Taasis za Kanisa la Waadventista


Wataalamu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato wametakiwa kutumia utaalamu wao katika masuala ya usalama kwenye mtandao,ubunifu wa program tumishi na program za komputa za utambuzi wa maeneo katika kufanikisha utume duniani.

Akitoa mada kwenye mkutano wa wataalamu wa intaneti wa kanisa la waadventista duniani (GAiN) ulioanza Februari 11 mwaka huu unaofanyika kwa njia ya mtandao na  unaoratibiwa toka Marekani yalipo makao makuu ya kanisa hilo na kuwakutanisha  washiriki toka nchi 70 duniani Mkurugenzi wa Teknohama wa Divisheni ya Marekani ya Kaskazini David Greene amewaasa wanateknohama kuhakikisha tovuti wanazosimamia na kuzitumia zina ulinzi wa kutosha.

Greene amesema kuwa asilimia  80 ya usalama wa tovuti utakuwa  umeondoka baada ya miaka miwili na hivyo kuna umuhimu wa kuhakikisha kuongeza usalama huo,na amewahimiza wataalamu wa tovuti za kanisa kuhakikisha wanapata vikoa vyenye usajili rasmi na vinavyotambuliwa kisheria.

Mkutano wa GAiN utamalizika  February 15,huku mada na mijadala mbalimbali ya teknohama  ikifanyika  mara tatu kwa siku kwa ajili ya kuwafikia washiriki walioko kwenye maeneo mbalimbali duniani ambapo unaweza kushiriki kwa kutembea katika tovuti ya gain.adventist.org na mada zilizojadiliwa zitawekwa baada ya majuma kadhaa ya mkutano huo. 

Wednesday, February 11, 2015

KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO RIVER SIDE ARUSHA LASHIKA NAFASI YA KWANZA BARANI AFRIKA KUTUNZA KUMBUMBUMBU ZA WASHIRIKI KITEKNOHAMA


 

Kanisa la River Side lililopo mtaa wa Njiro jijini Arusha, Tanzania, limetangazwa kuwa ni kanisa pekee barani Afrika ambalo limefikia asilimia 80 ya kutunza kumbukumbu za majina ya washiriki kwa kutumia mfumo wa kiteknolojia ya habari na mawasiliano  wa usimamizi wa makanisa ya kiadventista.Taarifa hiyo imetolewa  na Msimamizi mkuu wa mfumo wa Usimamizi wa makanisa ya kiadventista duniani Mrs Sherri Ingram-Hudgins Februari 9, mwaka huu wakati akitoa takwimu za mfumo mpya wa kanisa la Waadventista wa kusimamia makanisa (ACMS) kwenye mkutano wa wanateknohama wa kanisa hilo uliofanyika Maryland,Silver Spring,Marekani.

                                                                                                                                           

Takwimu hizo zinaonesha kuwa  Brazil ndio inaongoza duniani kuwa na washiriki wengi waliosajiliwa, ikifuatiwa na nchi za Peru na Argentina. Barani Afrika, Tanzania ndio inaongoza ikifuatiwa na Ghana.

Mwaka 2015, mfumo huu unategemewa kuanzishwa katika nchi za Kenya, Africa Kusini na Madagascar.


Akieleza mbele ya wajumbe kutoka division 13 duniani, Sherri alionesha jinsi mfumo huu wa kusimamia makanisa ulivyoboreshwa kwenye vipengele 5 ambapo unauwezo wa kutunza kumbukumbu za vikao vya kanisa mahalia, kupiga kura za kuchagua viongozi wa kanisa, unawezesha kanisa mahalia kuufasiri kwa lugha husika ya kanisa mahalia ,kutunza kumbukumbu za fedha za kanisa na kukusanya taarifa za kila idara kisha kuzituma konferensi, unioni, divisheni na Konferensi Kuu.Awali mfumo huu ulipoanza kutumika ulikuwa na uwezo wa kutunza majina ya washiriki na kuhamisha jina la mshiriki toka kanisa moja kwenda jingine. Sherri ametoa rai kwa wajumbe wote kuusimamia mfumo huu kwa makanisa yote makubwa yaliyopo mijini kisha kwenda makanisa yaliyopo vijijini.Divisheni ya  Afrika mashariki na kati iliwakilishwa na wajumbe watatu, Nicolas Washington (Kenya), Kelvin Opiyo (Kenya) na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Unioni Konferensi ya Kaskazini mwa Tanzania  Gideon Msambwa.