OnlineSaturday, January 24, 2015

MFUMO ENDESHI WA ANDROID ULIVYOANZA

 

Mfumo endeshi wa Android katika vifaa vya mawasiliano hasa simu ni miongoni mwa mifumo inayoonekana kufanya vyema na kutumiwa sana duniani kwa sasa.

Android ulioanzishwa ulivumbuliwa na Andy Rubin, Rich Miner, Nick Sears na  Chris White huko Palo Alto, California,Marekani walianzia mbali katika maendeleo yake.

Walikuwa wanalengo la kutengeneza programu za komputa kwa ajili ya kamera lakini baada ya kugundua kuwa kamera hazina soko kubwa waliamua kuanzisha kwa siri mfumo wa Android ili waweze kushindana na mifumo endeshi ya Symbiani na windows


Agosti 17,2005 kampuni ya Google ilihitaji japo waanzilishi hawa hawakufahamu kama kampuni hiyo ya mawasiliano ya intaneti itaweza kuingia katika soko la simu za mikononi kwa hapa ilipofikia.

Toka mwaka 2008, Android imekuwa ikitoa na kufahamika kwa matoleo yake ambayo ni Alpha 1.0, Beta 1.1, Cupcake 1.5, Donut 1.6, Éclair 2.0 – 2.1, Froyo 2.2 – 2.2.3, Gingerbread 2.3 – 2.3.7, Honeycomb 3.0 – 3.2.6, Ice Cream Sandwich 4.0 – 4.3.1, Jelly Bean 4.1 – 4.3.1, Kitkat 4.4 – 4.4.4 na Lollipop 5.0 – 5.0.2

MKUTANO WA WANATEKNOHAMA WAADVENTISTA KUFANYIKA KUPITIA MTANDAO WA INTANETI

 

Kanisa la Waadventista Wa Sabato mwaka huu litashiriki mkutano wa Waadventista watalaamu wa mawasilino ya Intaneti duniani (GAiN) kwa kuwakutanisha wataalamu hao kwa njia ya mtandao wa intaneti.

Mkutano huwa wa mwaka ambapo washiriki watakutana kutathimini huduma ya utume kwa kutumia teknojia itakuwa ni februari 11 hadi 15 kupitia tovuti ya  gain.adventist.org. na kila mada itawasilishwa na kufuatiwa na mijadala mbalimbali na itatangazwa mara tatu kwa siku ili kuwafikia watu wa kanda mbalimbali duniani. 


Waratibu wamesema kuwa wazo la kutumia mtandao ambalo linatazamiwa kuwezesha kupata washiriki wengi kutokana na mikutano mingine ya kanisa inayotarajiwa kufanyika mwaka huu.

Kwa mwaka huu mkutano wa wataalamu wa Teknohama utatolewa katika lugha za Kiingereza na kutafsiriwa moja kwa moja kwa Kifaransa,Kireno na Kiispaniola huku wito ukitolewa kwa washiriki kwa makundi kwenye makanisa,ofisini na nyumbani.

Miongoni mwa yatakayojadiliwa ni usalama kwenye mitandao,ubunifu wa program tumishi,elimu masafa,utalaamu wa masoko,utumiaji wa michezo ya komputa kwa injili na uendeshaji wa idara za teknolojia ya habari na mawasiliano kutokana na bajeti.


Waweza jisajili na kuona ratiba ya mkutano huo kupitia gain.adventist.org pia hushtag ya mkutano ni #GAiN15.

Saturday, January 17, 2015

WAKURUGENZI WA MAWASILIANO WA KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO WAASWA KUBUNI MIKAKATI

Mchungaji Lusekelo Mwakalindile akizungumza toja jijini Dar es salaam na wajumbe waliohudhuria mkutano wa mawasiliano uliofanyika Njiro Arusha kwa kutumia skype

 


Viongozi wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Tanzania katika idara ya mawasiliano wameaswa kubuni na mikakati ya kuwaelekeza washiriki namna sahihi ya utumiaji bora wa mawasiliano ikijumuisha mitandao ili kazi ya injili iende kwa kasi zaidi.

Wito huo umetolewa hivi karibuni na Mkurugenzi wa Mawasiliano kanda ya Afrika mashariki na Kati Mchungaji,Steven Bina katika ufungunzi wa kikao cha idara ya mawasiliano katika Unioni Konferensi ya kaskazini mwa Tanzania kilichofanyika  Njiro jijini Arusha kwasiku nne.

Aidha Mchungaji bina,amesema kuwa idara ya mawasiliano ndio idara inayounganisha idara zingine hivyo haina budi kuweka njia mbalimbali zinazoweza kuwaelekeza washiriki na wasio washiriki namna sahihi ya kutumia vyombo vya habari vya kanisa ili waone umuhimu wa vyombo hivyo ndani na nje ya kanisa.

 Mkutano huo uliwahusisha viongozi kutoka konferensi nne za union hiyo ambazo ni  konferensi ya kusini mwa Tanzania,konferensi ya kaskazini mwa Tanzania,konference ya magharibi mwa Tanzania pamoja na konferensi ya mara.

Wajumbe wa mkutano huo pia walifanya mazungumzo maalum ya Kimtandao kupitia kupitia mtandao wa kijamii wa Skype na Morning Star Radio na Tv kupitia wakurugenzi wa vituo hivyo vilivyoko jijini Dar es salaam, Ndugu Mazara Matucha wa Tv na Mchungaji Lusekelo Mwakalindile wa Radio,hii ikiwa ni katika kuboresha na kutatua changamoto zinazovikabili vyombo vya habari vya Kanisa hilo nchini.

 

Tuesday, January 6, 2015

WATAALAMU WABUNI PROGRAM YA SIMU INAYOTOA TAARIFA YA EBOLAWakati ugonjwa wa Ebola ukiendelea kuwa tishio katika baadhi ya nchi za Afrika magharibi, Wataalam wa afya nao wameendelea kuweka jitihada zaidi kuhakikisha kuwa wanaumaliza ugonjwa huo.

Katika jitihada zao hivi sasa wamebuni mpango wa mawasiliano ya simu ya mkononi wenye programu maalum inayotoa taarifa kutoka maeneo yaliyokumbwa na Ebola.

Programu hii ya simu imesambazwa katika maeneo mbalimbali nchini Guinea ambapo ugonjwa huu umesambaa kwa kiasi kikubwa, programu hii huweza kuonesha maeneo ambayo yako hatarini kuathiriwa naVirusi vya Ebola.

Shirika linaloshughulikia idadi ya Watu duniani, UNFPA linatoa elimu kwa wafanyakazi wa jumuia kuhusu namna ya kutumia programu hiyo inayowezesha kushirikisha taarifa kwa kwa wataalamu wa afya katika ngazi ya kitaifa na kimataifa.

Zaidi ya Watu 1,700 wamepoteza maisha nchini Guinea kutokana na Ebola