OnlineFriday, May 30, 2014

POLISI WA VISIWA VYA SOLOMONI WAUNGANISHA NGUVU KWENYE MAPAMBANO DHIDI YA UHALIFU MTANDAO

Polisi wa visiwa vya kifalme vya Solomon vilivyopo pasifiki ya kusini wameunganisha nguvu katika mapambano dhidi ya uhalifu mtandao na kuelezwa ya kwamba nguvu kubwa itasogezwa mashuleni ili kukuza uelewa wa maswala ya uhalifu mtandao (Awareness) na kusisitizwa hiyo ndio itakua shabaha yao ya awali.Taarifa iliyoandikwa na gazeti la kila siku la nchini humo kupitia tovuti yake.
 
Kupitia program ya mpango uliopewa jina la “Cyber safety pasifika” uliopangwa kuwasaidia watoto, vijana na wakubwa kutumia teknolojia katika hali ya usalama iliyojiri kuanzia mnamo tarehe 19 -25 May mwaka huu (2014) ulilenga kuhakiki matumizi salama ya mitandao visiwani humo unapewa kipaumbele na ukanda mzima wa pasifiki ya kusini kwa ujumla wake.

Makubaliano hayo yalifikiwa wakati wa mkutano ulio fanyika na kuwahusisha wakuu wa polisi wa visiwa hivyo. Kauli mbiu iliyo someka kama “ Historia yetu, Utamaduni wetu na mitandao yetu” Ilidahmiriwa kuhamasisha matumizi salama ya mitandao na simu katika ukanda huo wa pasifiki ya kusini.

Bi. Juanita Matanga
Bi. Juanita Matanga, Mkuu wa polisi wa visiwa hivyo aliainisha utayari wa kujipanga kukabiliana na uhalifu mtandao huku akitolea maelezo ukuaji wa kasi wa matumizi ya mitandao na simu katika visiwa hivyo na duniani kwa ujumla. Aidha Alieleza ukuwaji wa matumizi ya mitandao bahati mbaya wengi hawajui athari zake. Hilo ndilo lililo wasukuma kuanzisha kampeni hiyo ya kukuza uelewa wa maswala ya uhalifu mtandao (Cybercrime Awareness Campaign) visiwani humo.

Matanga alisisitiza kampeni hiyo itakua endelevu na pia kutakua na kupitia sharia zilizopo ili kuweza kuziboresha kuhimili makosa ya uhalifu mtandao. Alianisha pia katika visiwa hivyo bado ukuaji wa kasi wa makosa ya kimtandao haujaanza kuonekana na polisi visiwani humo wako katika kuhakiki wanakuza uelewa kwa raia wake ili kuweza kukabiliana na hali hiyo – Kuzuia tatizo ni bora zaidi kuliko kusubiri tatizo litokee ili kuanza kukabiliana nalo.

Mkuu huyo wa polisi alianisha pia yakua nchi nyingine za ukanda huo wa pasifiki  tayari wamesha kua na taratibu wa kuhamasisha matumizi bora ya mitandao kukabiliana na uhalifu mtandao (Cybercrime awareness programs)  na umefika wakati visiwa hivyo navyo kuingiza taratibu hiyo katika vitendo na kusisitiza tena kua swala hilo litakua  endelevu.
Na:Yusufu Kileo

TAPELI ATUMIA SIMU YA MKONONI KUTAPELI USAILI IDARA YA UHAMIAJI MAKAO MAKUU

Mtu mmoja ambaye alijitambulisha kwa cheo cha Katibu wa Usaili Idara ya Uhamiaji Dr Mawazo Kaburugu anatafutwa na idara hiyo kwa tuhuma za kutoza watu sh 10,000 kwa njia za udanganyifu.

Mtu huyo ambaye alifanikiwa kutuma ujumbe kwa watu zaidi ya 900,wanaotaka kufanyiwa usaili kwenye idara ya Uhamiaji,anadaiwa kupata kiasi kikubwa cha fedha kutokana na ujumbe aliokuwa akutuma kwa watu hao.

Ujumbe huo ulisomeka "Habari ndugu,pongezi kwa kuitwa kwenye usaili kuanzia tar 9/6.Idara ya uhamiaji inakufahamisha kuwa unatakiwa kulipa sh 10,000 na haitarejeshwa kama gharama za usaili vikiwamo vitambulisho pekee ndio wataruhusiwa kuingia ukumbini,malipo yote yatumwe kwa tigo pesa kwenye namba 0715 54 62 81 kuanzia tarehe 26 hadi 30,kisha tuma sms yenye code za Tigopesa na jina lako kamili,imetolewa na Kamishna Dr Mawazo Kaburugu Katibu wa Usaili".

Mwandishi wa gazeri la Raia Tanzania aliwasiliana na mtu huyo ambapo alieleza kuwa wote ambao wameitwa kwenye usaili watume fedha hiyo kama ujumbe ulivyotolewa na kuongeza kuwa pesa hiyo inahitajika haraka sana ili iweze kufanyakazi iliyokusudiwa kwa ajili ya usaili.

Kaimu Mtendaji wa Idara ya Uhamiaji,Tatu Bruani amesema mtu huyo ni tapeli na ambao wametumiwa ujumbe wasitume pesa hizo.
Chanzo:Gazeti la RaiaTanzania

EPZA NA COSTECH WAINGIA MKATABA WA KUKUZA TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO NCHINI TANZANIA

Mamlaka ya Ukanda Maalumu ya Uwekezaji nchini Tanzania (EPZA)na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) wameingia kwenye makubaliano ya kukuza teknolojia ya habari na mawasiliano nchini humo.

Makubaliano hayo yalifanywa na Mkurugenzi wa EPZA,Dr Adelhelm Meru na wa COSTECH,Dr Hassan Mshinda jijini Dar es salaam hivi karibuni.

Akizungumza baada ya utiaji saini huo,Dr Meru alisema hatua hiyo ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi,ambapo eneo la EPZA lililoko Bagamoyo litatumika kwa ajili ya kuligeuza kuwa kituo kikubwa cha maswala ya TEKNOHAMA Afrika Mashariki na Kati.

Amesema eneo hilo lenye ekarai 238 litaendelezwa kwa ushirikiano wa taasis hizo mbili kujenga miundombinu ya maji,barabara na umeme hivyo kuvutia uwekezaji wa kampuni kubwa duniani za DELL,IBM,MICROSOFT na HP kuwekeza.

Thursday, May 29, 2014

ANGALIA VIDEO HII YA GARI LISILO NA DEREVA

Wednesday, May 28, 2014

GOOGLE KUUNDA MAGARI YANAYOJIENDESHA.


 


Kampuni ya Teknolojia ya Google imesema itaanza kutengeneza magari yasiyohitaji madereva.

Kampuni hiyo ambayo imejijengea sifa kwa njia ya kipekee ya utendakazi wake katika sekta ya kiteknolojia imekuwa ikikarabati magari ya kawaida.

Magari bila Usukani
  Litakuwa linaendeshwa kwa kubofya tu.
Google imesambaza picha ya gari hilo ambalo inasema ni la kutumiwa mijini na linapaswa kuwa chambo kwa wale ambao bado hawana imani na teknolojia hii ya hali ya juu.

Gari linalojiendesha

Muasisi wa kampuni hiyo Sergey Brin alizindua gari hilo la kipekee katika mkutano na wanahabari huko California.
Brin alisema kuwa teknolojia hiyo inauwezo mkubwa wa kuimarisha maisha ya watu .

Watafiti wa magari yanayojiendesha yenyewe bado wanajadili iwapo kuwepo kwa magari hayo mabarabarani yatakuwa na upungufu wowote ikiwemo dhana kuwa itachangia ongezeko la msongamano wa magari.

Chanzo:BBC

Friday, May 23, 2014

MKWEZI AOKOLEWA MAUTI NA FACEBOOK

John All aliyeokolewa na facebook
 Mkwezi wa milima mirefu ameokolewa kutoka futi 80 bondeni alipoandika ''Nahitaji msaada'' katika mtandao wa Facebook

Profesa huyo wa jiografia aliwaambia marafiki zake wa Facebook kuwa alikuwa ameanguka ndani ya bonde la Himalaya umbali wa futi 19,600 kwenda chini.

Kwenye ukurasa wa facebook wa ‘'American Climber Science Program’' baada ya kuanguka kwendye bonde hilo. All mwenye umri wa miaka 44 aliteguka bega, kuvunja mbavu tano, goti, na kiwiko. 

All aliandika, ‘’ tafadhali muwafahamishe waokoaji wa Global, John amevunjika mkono, mbavu na huenda anavuja damu ndani ya mwili. Tafadhali harakisheni’’

Marafiki wake wa Facebook waliona video ya All akiwa na majeraha na kuwajulisha waokoaji kilichokuwa kikitendeka na kisha kuwasisliana na All na kumwambia kuwa atapata msaada.

Baada ya saa kadhaa, All aliandika kwenye ukurasa huo wa Facebook kuwa waokoaji hawangeweza kumpata kwa kutumia helikopta kwa hivyo angejitahidi ingawa kulikuweko na baridi na alikuwa na maumivu 
mengi.
Baada ya saa 19, profesa All aliokolewa na kupelekwa hospitalini mjini Kathmandu ambako anapata matibabu.
Chanzo:BBC

TANZANIA IMEOMBA MKOPO WA DOLA MILIONI 154 TOKA INDIA KWA AJILI YA UJENZI WA MINARA YA SIMU

Serikali ya Tanzania imeomba mkopo wa Dola za Marekani milioni 154 ambazo ni takribani shilingi za kitanzania bilioni 246 kwa India kuwezesha ujenzi wa minara ya mawasiliano ya simu katika maeneo yasiyo na huduma hiyo,ambapo sh.bilioni 320 zinatarajiwa kutumika.

Tayari Serikali imeorodhesha maeneo yanayotakiwa kuwekewa minara na gharama zake ikiwa ni hatua ya kuwezesha kuanza utekelezaji wa ujenzi huo.

Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia,January Makamba amesema bungeni jana wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Bukene,Selemani Zedi (CCM) aliyetaka kujua juhudi za Serikali kujenga minara katika sehemu zisizo na mawasiliano,hususani yasiyo na mvuto wa kibiashara.

Makamba pia amesema kupitia mfuko wa mawasiliano kwa wote ulioanzishwa na Wizara hiyo utasaidia kuharakisha kazi hiyo ya upelekaji huduma za mawasiliano.

Takwimu zilizotolewa na jana na Kampuni ya Simu ya Vodacom zinaonesha kwamba Kenya inaongoza kwa mawasiliano ya mawasiliano ya simu na intaneti kwa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara ikifuatiwa na Tanzania,Uganda,Rwanda na Burundi.

Takwimu hizo zinaeleza kuwa julai mwaka jana Kenya yenye wakazi milioni 44,inawatumiaji wa simu za mkononi milioni 34.4 huku intaneti wakiwa ni milioni 16.3 sawa na asilimia 41.

Tanzania inafuata kwa kuwa na wakazi wapatao milioni 48.3 na watumiaji wa simu za mkononi ni milioni 27.4 na wanaotumia intaneti ni milioni 5.31 sawa na asilimia 11 tu
 

Wednesday, May 21, 2014

SERIKALI NCHINI CHINA IMEPIGA MARUFUKU MATUMIZI YA WINDOWS 8 KWA KOMPUTA ZOTE ZA SERIKALI


Nchini China kumezuka gumzo baada ya serikali kupiga marufuku matumizi ya Window 8 katika computa zote za serikali nchini humo. Taarifa iliyo chapishwa na CHINA DAILY” ilibainisha uamuzi huo wa serikali uliowekwa kwenye tovuti ya serikali ya nchini humu ambapo ilisisitiza zoezi hilo hali husu komputa za watu binafsi isipokuwa zile zinazotumiwa na serikali.

Tangazo hilo la serikali linalosemeka “HAPA” limebainisha uamuzi huo wa serikali umekuja baada ya kufungiwa huduma za kiusalama kwa Window XP huku likiweka wazi ya kuwa wamefikia hapo kutokana na sababu za kiusalama mtandao. Komputa hizo za serikali zitakua ziki tumia Operating system nyingine yoyote isipokua Window 8 ilisistizwa.

Kwa sasa nchini uchina inasemekana Komputa nyingi za serikali zilikua zinatumia Window Xp ambayo imekua si salama tena kimtandao ambapo inaweza ruhusu mhalifu kupenya na kuleta madhara kwa mtumiaji hivyo kuongeza wimbi la uhalifu mtandao kwa sasa, hususan watumiaji wa Window hiyo iliyositishiwa huduma kwa sasa.

Kwa upande wa Microsoft, Imeonyehsa mshangao kuwa window 8 imeonywa kutumika nchini humo ilhali wanaamini iko salama na wanaipatia huduma zozote za kiusalama kila inapo hitajika, Msemaji wa Microsoft alinukuliwa akisema hivyo na kusisitiza ya kuwa Microsoft imekua ikitumia nguvu ya ziada kuhakiki bidhaa zake na huduma zake zinafikia kiwango cha matumizi kwa mujibu wa mahitaji ya serikali.
Uchina imeonyesha dhamira yake ya kuongeza nguvu katika kutengeneza Operating system zake zenyewe, huku Bwana Qi Xiangdong, raisi wa Qihoo 360, akieleza ni muda muafaka kwa makampuni ya nchi hiyo sasa kukuza utengenezaji wa operating system zake.


Kwa upande wa balozi wa uchina nchini marekani amesita kutoa kauli ya haraka ikizingatiwa kuwepo na hali isiyo njema inayo husiana na maswala ya kiusalama mtandao kwa nchi hizo mbili ( Marekani na Uchina)

Saturday, May 17, 2014

ANGALIA VIDEO JINSI YA KUWA SALAMA NA WAHALIFU KUPITIA MITANDAO

Thursday, May 15, 2014

NCHINI KENYA:WANAOTUMA UJUMBE WA NGONO KWA SIMU NA MITANDAO KUFUNGWA JELASerikali ya Kenya imesema watu watakaopatikana na hatia ya kutuma ujumbe wa kingono kwa kutumia simu za kiganjani na intaneti watafungwa Jela.

Adhabu hiyo itawahusu wale wanaotuma ujumbe wenye picha za watu walio uchi na zenye mada ya ngono nchini humo.

Maafisa wakuu wa serikali wanasema kuwa yeyote atakayepatikana na hatia atafungwa jela kifungo cha miezi mitatu kwenda chini.

Afisa mkuu kutoka tume ya mawasiliano ya Kenya , Christopher Wambua, ameviambia vyombo vya habari nchini humo ,kwamba watu wenye tabia hiyo ya kutuma ujumbe wa kingono ,pamoja na picha zenye watu walio uchi ,watatozwa hadi shilingi elfu hamsini za Kenya au dola miatano na themanini na nane za kimarekani sawa na shilingi laki tisa arobaini elfu na mia nane za kitanzania kama faini au kufungwa jela.

Onyo hilo litawahusu hasa wale walio na uzoefu wa kutumiana ujumbe kama huo kupitia kwa simu ya kiganjani au kwenye intaneti.  

Kwa mujibu wa taarifa za serikali, kiwango ambacho watu hutumiana ujumbe wenye mada ya ngono pamoja na picha za watu walio uchi, zao wenyewe au za mtu mwingine kwa simu zao za kisasa ilipanda hadi asilimia sitini.
Chanzo:BBC

Saturday, May 10, 2014

DONDOO TANO ZA KUJILINDA KWA SIMU AINA YA IPHONE

TAKWIMU ZA NJIA ZA MAWASILIANO YA KIMAHUSIANO KATIKA ULIMWENGU WA DIGITALI

Communicating Love in the Modern Era
Explore more visuals like this one on the web's largest information design community - Visually.

Saturday, May 3, 2014

WAHALIFU WATUMIA MITANDAO KUHADAA WATU KIMAPENZIPolisi nchini Ufilipino, wamesema kuwa wamewakamata washukiwa wa uhalifu katika mitandao ambao ni sehemu ya kikundi cha watu wanaowahadaa watu kwenye mitandao ya kijamii kote duniani.

Washukiwa hao huwashawishi watumiaji wa Internet au walengwa wao katika nchi za kigeni kujipiga picha wakiwa uchi na wakiwa katika vitendo vya mapenzi na kujirekodi kisha kuwatumia.
Wahalifu hao baadaye hudai kiasi Fulani cha pesa kutoka kwa walengwa la sivyo huwatishia kuwa watawatumia jamaa wao picha na video hizo.

Polisi wamefanikiwa kuwakamata washukiwa 58 katika operesheini hiyo iliyohusisha polisi wa kimataifa Interpol.

"Lengo la washukiwa hawa ni kutengeza akaunti kwenye mitandao ya kijamii kwa lengo la kuwatafuta wateja wao hasa wazee katika nchi za kigeni,’’alisema afisa mmoja wa polisi.
"Katika akaunti zao hizo wao hujidai kuwa ni wasichana wenye asili ya Asia wanaotafuta wapenzi katika nchi za kigeni.’’

"Baada ya kujuana vyema na watumiaji wa mitandao wasiojua kuwa wanahadaiwa, wao huwakaribisha kuwa marafiki zao kwenye mitandao , kuwasiliana nao kwa njia ya video kwenye mitandao hiyo hiyo na kisha kufanya nao vitendo vya mapenzi kupitia kwa kompiuta huku wakirekodi kila kinachofanyika. ‘’

Kanda hizo sasa hutumiwa kama njia ya kupata pesa kutoka kwa waathiriwa kwa kutumia vitisho kuwa watasambaza kanda hizo kwa watu wa karibu wa waathiriwa la sivyo walipwe kati ya dola 500 na 2,000. Pia hutishia kusambaza kanda hizo kwenye mitandao ya kijamii.

Afisa mkuu wa Interpol amesema kuwa uhalifu huo umeenea sana kwenye mitandao. Uhalifu wa aina hii hauna mipaka umeenea kote , sio Ufilipino peke yake.
Chanzo:BBC-SWAHILI

HALMASHAURI YA KINONDONI YANUFAIKA NA ULIPAJI WA KODI KWA KUTUMIA SIMU ZA MKONONI NA MAX-MALIPO

Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imeleza kuwa imenufaika na utaratibu mpya wa utaratibu wa ulipaji wa kodi kwa kutumia huduma ya simu za mkononi na Max-malipo.

Taarifa iliyotolewa hivi karibuni na Afisa Uhusiano wa Manispaa ya Kinondoni Sebastian Modestus Mhowera imeeleza kuwa huduma hiyo mpya inayotolewa kupitia mfumo unaojulikana kama “e–payment system”,ambao unamwezesha mwananchi kulipa kodi yake muda wowote, kwa haraka na urahisi na mahali popote.

Huduma hii inatolewa na Manispaa kwa kushirikiana na wakala anayetambulika kama “Max-malipo” ambaye kupitia huduma zake mitaa 171 iliyopo katika Kata 34 imeunganishwa katika mifumo hiyo ya ulipaji kodi.


Mfumo huu wa ukusanyaji wa kodi ndani ya Manispaa ni hatua ya utekelezaji unaozingatia maelekezo ya waraka wa Serikali Na. 5 wa mwaka 2009 unaohamasisha matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEKNOHAMA) kwa lengo la kurahisisha utoaji wa huduma kwa Umma, kwa ufanisi na kwa wakati.
 

Taarifa inaeleza kuwa manispaa hiyo iliona ni vema ikaingia katika utaratibu huu ili mwananchi aweze kulipia kodi popote kwa kutumia Max-malipo au wakala wa simu za mkononi yaani Tigo pesa Na. 212888 na M-Pesa Na. 212888.

Katika kipindi kifupi cha muda wa miezi 3, tangu mfumo huu mpya ulipoanzishwa rasmi kumekuwa na

• Ongezeko la ada ya kuchangia huduma za Afya (Cost sharing) imeongezeka kutoka Tshs. 45,000,000/= kwa wiki hadi kufikia Tshs. 65,000,000/= kwa wiki, sawa na ongezeko la 69%

• Chanzo cha kodi ya majengo hadi mwishoni mwa Machi zilikusanywa Tshs. 339,000,000/= tofauti na awali ambapo hadi kipindi kama mwaka 2013 zilikuwa kwa  ongezeko la asilimia 269 hiki Tshs. 126,000,000/=

• Maeneo mengine ongezeko la mapato limezidi bajeti ya mwaka iliyotakiwa kukusanywa. Kwa mfano katika ushuru wa huduma za jiji (City Service Kavy) ambapo tumezidi kwa 18%

• Ushuru wa Masoko umeongezeka kwa wastani wa asilimia 20 ya lengo la kila mwezi.

• Lesseni za biashara hadi Machi zilikusanywa shs. 2.4 Bilioni sawa na 93% ya bajeti ya Manispaa ya chanzo hiki ya shilingi. 2.6 Bilioni kwa mwaka.