OnlineThursday, February 27, 2014

MJADALA KUHUSU MITANDAO YA KIJAMII KUTOKA JAMII PRODUCTION


Karibu katika kipindi hiki cha kwanza cha moja kwa moja (Live) kilichorushwa toka studio zetu za Washington DC
Katika kipindi hiki, mjadala ulikuwa juu ya MITANDAO YA KIJAMII.
Washiriki walikuwa Prof Nicholas Boaz. Mwalimu wa Mawasiliano kutoka Chuo kikuu cha Maryland.
Mzee Emmanuel Muganda. Mtangazaji mkongwe aliyefanya kazi zaidi ya miaka 30 katika Idhaa za Sauti ya Amerika (VOA) na pia Denzel Musumba. Mmiliki wa Border Media Group ambaye kwa miaka mingi amekuwa akitangaza kupitia mitandao ya kiJamii
Kwa njia ya Skype tuliungana na Jeff Msangi. Mwandishi, Blogger na mwanaharakati aliyejiunga nasi kutoka Ontario Canada
Na kutoka nchini Tanzania tulimsikia mwakilishi wetu Ahmad James Nandonde aliyeongea na Mkuu wa Mkoa wa Mara na watu wengine.
Karibu sana

NB: Tunaomba radhi kwa ubora hafifu wa sauti katika baadhi ya sehemu za kipindi.

FAIDA ZA MTAMBO WA USIMAMIZI NA UHAKIKI WA MAWASILIANO YA SIMU ULIOZINDULIWA LEO JIJINI DAR ES SALAAM.

Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dr Jakaya Mrisho Kikwete amezindua Mtambo Maalum wa Usimamizi na Uhakiki wa Mawasiliano ya Simu, Februari 27,2014 jijini Dar es salaam,uzinnduzi uliofanyika yalipo makao makuu ya Mamlaka ya Mawasilino Tanzania (TCRA)

TCRA kupitia Mkurugenzi wake Profesa John Nkoma ameeleza mtambo huo utakuwa na faida zifuatazo;

1.Kuwa na uwezo wa kujua mapato yanayopatikana kwenye simu za kimataifa zinazoingia nchini.

2.Kuongeza mapato kwa sekta ya mawasiliano kutokana na wapigaji wa simu waliopo nje ya nchi ili kuweka  uwiano ulio sawa kati ya makampuni ya hapa nchini na yale ya nje ya nchi.

3.Kuwa na utaalamu wa kuweza kuzuia matumizi ya simu zinazopigwa nchini na makampuni yasiyo na leseni kwa ajili ya kuunganisha simu za kimataifa na hivyo kuikosesha serikali ya Tanzania na Makampuni ya simu mapato halali.

4.Kuongeza uwazi na uwajibikaji katika sekta ya mawasiliano.

5.Kuipa serikali kwa kupitia TCRA uwezo wa kuweza kusimamia sekta ya mawasiliano vizuri,kwa kuwa sekta inakuwa kwa kasi na inatoa huduma nyingi sana zikiwemo za benki mtandao.

Makampuni yenye leseni za kutoa huduma za simu za kimataifa na nchini Tanzania ni Airtel,MIC (Tigo),Sixtelecoms,TTCL,Vodacom na Zantel
ANGALIA VIDEO YA RAIS WA TANZANIA JAKAYA KIKWETE ALIPOZINDUA MTAMBO WA USIMAMIZI NA UHAKIKI WA MAWASILIANO YA SIMU FEB 27,2014

Monday, February 24, 2014

BBM WATOA AHADI YA KUPATIKANA KATIKA SIMU ZA NOKIA NA WINDOWS

 

Watumiaji wa simu za Nokia na Windows wamekuwa wakitamani kutumia huduma ya ujumbe wa maneno ya BlackBerry  (BBM) huduma hiyo sasa itapatika katika simu hizo.

 Nokia na BlackBerry wamethibitisha mapema leo kuwa huduma hiyo ya ujumbe wa bure imekubalika na  na itatumika katika simu za Nokia na Lumia zenye mfumo wa Windows na katika simu mpya ya Nokia iitwayo Nokia X ambayo imetengenezwa katika mfumo wa Androd.

BlackBerry imesema kuwa huduma hiyo itaanza kutumika miezi michache ijayo na itaanza kupatikana katika Nokia Store.

Hatua hii iliyochukuliwa na BlackBerry,Nokia na Microsoft wakati ambapo Facebook imetumia dola $19 kununua programa tumishi ya ujumbe wa maneno ya Whatsapp.

Huduma za BBM na  Whatsapp)  zimepata umaarufu sana katika mawasiliano kwa watu mbalimbali kwa urahisi zaidi.

Saturday, February 22, 2014

MAARIFA: NAMNA YA KUTAFUTA TAARIFA UNAZOHITAJI KWA MUDA MFUPI KUPITIA GOOGLE HII HAPA

Intaneti ni bahari kubwa yenye taarifa nyingi,kwa hiyo kupata taarifa unayoitafuta ni lazima uuelekeze utaratibu wa intaneti unaotafuta mambo mbalimbali ili kukupatia taarifa sahihi unayoitaka.

Kwa kuwa tovuti ya google imekuwa ikitumiwa sana duniani katika kutafuta taarifa mbalimbali hapa kuna mbinu rahisi zitakazokusaidia kupata taarifa sahihi unazozitafuta kwa muda mfupi.

1. Use of Quotation Marks and Key Phrases

When looking for something on Google, envelope the key word with quotation marks to instruct the search engine to bring all about what you searching for. For example if you type in"Reebok", search engine would bring all about Reebok and nothing else.

2. Time Range Search


If you want to know about the NFL between 2011 to 2014 for example your search would look like this NFL 2011...2014. This would instruct the search engine to bring up all about the NFL between 2011 and 2014.

google-search-tricks

3. Document Type Search

If you are looking for a particular file type say a PDF file for example you can instruct Google to look for PDF files on Technology by typing in "Filetype: PDF Technology". For word file replace PDF with docx, for PowerPoint files put in ppt, for excel type in xls.4. Inclusive Search

If you want search engine to bring up two terms in the search, like Apple and Mac for example, just type Apple OR Mac.

5. Searching for Word Definition

You don't need to type a word on Google and start looking for dictionary definition on dictionary sites. To get a definition on Google just type "define: word" and the definition would pop up on top page.


6. Make Calculations

You could do your maths calculation if you know how to use your symbols properly. You could make calculation direct from Google by using + - ( ) * to do your basic maths.


7. Unit & Currency Conversion Search


When search for a unit conversion, type in the command telling the search engine what to convert and to what. for example "1 dollar in Naira"


8. Using Wildcards

When you have partial information about something and want to get full  details about the matter, use wildcards such as asterisk (*) to fill the missing fields. For example if you want to know properties Gogle bought and how much, your search would look like this "Google acquired * for *".

-Maelezo zaidi tembelea hapa: http://www.randietech.com/2014/02/google-search-tricks-and-tricks-how-to.html#sthash.xWrfP8fy.dpuf

Friday, February 21, 2014

FACEBOOK KUINUNUA WhatsApp KWATENGENEZA MABILIONEA WAPYA KATIKA TEKNOHAMA

 


Mtandao wa kijamii wa Facebook umenunua programu tumishi ya huduma za ujumbe mfupi wa maneno ya WhatsApp kwa dola za marekani bilioni 19 (TSh 30.9 trilioni) katika taarifa iliyotoka mapema Februari 19,2014.

Ununuzi huo wa WhatsApp umetengeneza mabilionea wapya angalau watatu, akiwemo mwanzilishi wa WhatsApp, Jan Koum, ambaye atajiunga na bodi ya wakurugenzi ya Facebook.

Mwanzilishi mwenza wa WhatsApp, Brian Acton, naye anaingia katika orodha ya mabilionea wapya vijana.

Miaka 4 iliyopita, Acton alijaribu kuomba kazi Facebook na Twitter baada ya kupunguzwa kutoka Yahoo,inaandika  blogu ya teknolojia ya Techcrunch.
 .
Leo hii, program aliyoitengeneza na rafikiye wa Yahoo, Koum, inagombaniwa na kampuni zilezile zilizomkataa na hatimaye, imenunuliwa kwa mabilioni ya dola na Facebook.

Wengine walioula ni wawekezaji wa kwanza wa WhatsApp toka kampuni ya uwekezaji ya Sequoia.

Techcruch inaripoti vijana wa Sequoia wametengeneza zaidi ya dola bilioni 3 (TSh 4.9 trilioni) – mara 50 ya pesa waliowekeza – katika ‘dili’ hilo.

Facebook, ambao ni mtandao wa kijamii  mkubwa kuliko yote duniani ukiwa na wanachama zaidi ya bilioni 1, inaamini kuwa WhatsApp itasaidia kuongeza uwepo wake katika masoko mbalimbali duniani, hasa katika nchi zinazoendelea za Afrika, Asia na Amerika Kusini ambapo teknolojia ya simu za mkononi imeshika hatamu.

Uamuzi huo unaipa Facebook nafasi ya kuongeza idadi ya watumiaji wa mtandao wake, itarithi zaidi ya watumiaji milioni 450 wa WhatsApp.

Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Facebook, Mark Zuckerberg anaamini uamuzi wa kuinunua WhatsApp kwa dola bilioni 19 ni wa busara, kwa kuwa “[WhatsApp] ni mtandao unaokuwa kwa haraka, ambayo itafikia watumiaji zaidi ya bilioni moja hivi punde.”
 
WhatsApp iliyoanza kutumika mwaka 2009,hadi kufikia  November 10, 2013, ilikuwa na watumiaji milioni 190 kwa mwezi,wakiwa wametumiana picha milioni 400 kila siku, ambapo iliweza kuhifadhi ujumbe wa maandishi bilioni 10  kwa siku.

Desemba 2013 WhatsApp ilieza kuwa ilikuwa na watumiaji milioni 400 kila mwezi. 

Program huyo tumishi kwa sasa inatumika katika vifaa vya mawasiliano yaani tabiti,simu na kompyuta zenye mifumo ya iOS,Android,BlackBerry,Simbiani na Windows
 
Chanzo:Gazeti la Mwananchina na Wikipedia org

Wednesday, February 19, 2014

AWAMU YA PILI YA UZIMAJI WA MITAMBO YA MFUMO WA UTANGAZAJI WA ANALOJIA KUANZA MACHI 2014 NCHINI TANZANIAMamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) inakusudia  kuanza awamu ya pili ya uzimaji wa mitambo ya mfumo wa utangazaji wa analojia kwenda dijitali katika miji ya Singida na Tabora mwishoni wa mwezi Machi 2014.

Miji mingine katika awamu ya pili itakuwa Musoma, Bukoba, Morogoro, Kahama, Iringa, Songea na Lindi. Awamu hiyo inategemewa kukamilika mwishoni mwa mwezi Oktoba 2014.

Taarifa ya TCRA kwa vyombo vya habari ilitolewa jana na Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Prof John Nkoma inasema  nia ya Mamlaka ni kuona zoezi la uhamaji kutoka mfumo wa utangazaji wa analojia kwenda mfumo wa kidijiti linakamilka nchini humo  kabla ya kufikia ukomo wa matangazo ya analojia kama ilivyoelekezwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia Mawasiliano Duniani (ITU) juni 17,2015.

Tanzania ni nchi ya kwanza kuzima mtambo ya analojia Barani Afrika, Zoezi la uzimaji mitambo kwa awamu ya kwanza iliyoanza disemba 31,2013 ambalo lilifanyika kwenye miji saba lilikuwa na changamoto nyingi, kwani liligusa nyanja mbalimbali zikiwemo za kijamii, kibiashara, kiufundi na Kisiasa.

MAARIFA:JINSI YA KUBLOCK MAWASILIANO KWENYE VIBER
 

Unapomblock mtu kwenye viber inamaana umezuia kuwasiliana na mtu yoyote kwa njia yoyote katika mtandao wa kijamii wa viber,hutapokea ujumbe wa maneno ama kwa kupiga simu.
 Hii inamaanisha kuwa

 • Hutaweza kupiga simu ama kuwasiliana kwa ujumbe wa maneno.
 • Picha ya wasifu wako na hali yako vitaonekana kwa uliyemblock.
 • Ukijaribu kurudisha tena mawasiliano hutaona ujumbe ama kumbukumbu ya simu ulizopiga kabla ya kublock.
 • Kublock hakutafuta ujumbe na historia ya mawasiliano yaliyofanyika mwanzo kabla
 • Kumblock mtu hakutamzua mtu huyo kukuongeza kwenye mawasiliano ya makundi anayowasiliana nayo yaliyoundwa katika mtandao wa Viber

Nawezaje kublock mawasiliano?

Kuna njia mbalimbali.

 1. Unapopata ujumbe toka kwa mtu usiyemfahamu,ukurasa wa mawasiliano utaonesha chaguzi mbili,unaweza mwongeza katika orodha ya unaowasiliana nao ama unaweza kumblock When receiving a message from an unknown contact.  
 • Unapoblock mtu kwenye kundi,unaweza kufanya hivyo kwa watu waliopo kwenye kundi hilo nenda kwenye kundi chagua contact  > chagua menu ya kifaa chako > nachagua  "Block".
 • Uliyemblock ataendelea kuona unachokifanya kwenye kundi husika na wewe unaona pia.
 • Njia hii itatumika moja baada ya mawasiliano mengine unayoyafanya.  
2.    Kublock namba uliyoihifadhi
 • Unaweza kublock kwa ukurasa wa maelezo ya mawasiliano kwa kupeleka kushoto mwa kioo cha kifaa chako cha mawasiliano chagua menu > Chagua "Block"
 • Unaweza kuweka namba kwa kufuata hatua hizi  settings > Privacy > Block List > Block number. Kumbuka kuweka namba kwa kufuata utaratibu huu  + namba ya nchi – Namba ya eneo – Namba ya simu. Mfano kwa namba ya Tanzania itaonekana + 255 123 456 789 

Unawezaje kurudisha ulichokiblock?
 1. Chagua menu ya  More Options
 2. Chagua Settings
 3. Ingia Privacy
 4. Chagua Block List
 5. Tafuta namba unayotaka kuirudisha
 6. Chagua Unblock
Kumbuka namba unayoirudisha haitarejesha ujumbe uliotumwa wakati ilipoiblock

Unapoblock namba ya mtu katika wasifu wako wa viber,mhusika hatagundua hili ataendelea kukutumia ujumbe na ujumbe huo hautaupata.  

Kwa ajili ya kuwa na faragha hakuna njia moja inayoonesha kuwa mtu amekublock ama la,inabaki tu kwamba ukiblock namba ya mawasiliano mtu hata jua na hata wewe ukifanyia hivyo hutajua.