OnlineSaturday, September 28, 2013

SEMINA YA ACMS YAMALIZIKA

Semina kuhusu mfumo wa utunzaji wa taarifa za washiriki katika Kanisa la Waadventista Wa Sabato (ACMS) imemalizika jijini Arusha Septemba 26,2013.

Semina hiyo iliyohudhuriwa na Makatibu wakuu pamoja na Wakuu wa Teknohama kutoka majimbo yote ya Kanisa la Waadventista Wa Sabato nchini Tanzania imekuwa na mafanikio makubwa kutokana na wahusika wote kuhudhuria kikamilifu. 

Akizungumza katika kuhitimisha semina hiyo, Msimamizi wa mfumo huo kutoka Makao Makuu ya Kanisa la Waadventista Wa Sabato Ulimwenguni Bi. Sherri Ingram-Hudgins, ametoa shukrani zake kwa Uongozi wa Tanzania Union pamoja na washiriki wote wa semina hiyo kwa ushirikiano waliouonyesha kwa muda wote wa semina.

Pia Katibu Mkuu wa Tanzania Union, Mchungaji Davis Fue, amewashukuru wakufunzi pamoja na wote waliohudhuria semina hiyo, huku akiwataka Makatibu Wakuu pamoja na Wakuu wa Teknohama kuharakisha upatikanaji wa taarifa za washiriki wa Kanisa ili matumizi ya mfumo huo yaanze kwa ufanisi.

Mfumo huo uliobuniwa na wataalamu watano wa program za komputa unakadiliwa kutumia dola za kimarekani milioni 5.

Sherri Ingram-Hudgins ambaye ni msimamizi wa mfumo wa ACMS kutoka Makao Makuu ya Kanisa la Waadventista Wa Sabato Ulimwenguni akitoa maelezo ya kuhitimisha semina hiyo.

Mr. Haggai Abuto ambaye ni Mkuu wa Teknohama kutoka Divisheni ya Afrika Mashariki na Kati akitoa shukrani zake katika kuhitimisha semina hiyo.

Mchungaji Davis Fue ambaye ni Katibu Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato, Tanzania Union akitoa shukrani zake katika kuhitimisha semina.

Washiriki wa semina ambao ni Makatibu Wakuu na Wakuu wa Teknohama wakiwa katika picha ya pamoja.

Saturday, September 21, 2013

ANGALIA VIDEO YA NAMNA UNAVYOWEZA KUWASILIANA KWA KUTUMIA GOOGLE HANGOUTS

ANGALIA TEKNOLOJIA YA KUCHAJI IPHONE KWA KUTUMIA PUMZI

FACEBOOK WATAKA KUJUA MAANA YA KINA YA PACHIKO LAKO
Facebook imeanza kutumia   teknolojia iitwayo  akili bandia (AI) inayotambua maana ya kina ya pachiko la mtumiaji wa mtandao huo wa kijamii.

Mbinu hii itaweza kusaidia  Facebook kuwaelewa  watumiaji wake na data zao zilizo bora.

Facebook imeweka utaratibu huo ili kufahamu vyema watumiaji milioni 700  ambao hushiriki maelezo ya maisha yao binafsi kwa kutumia mtandao jamii kila siku.

Kikundi cha watafiti wapya  ndani ya kampuni hiyo inafanyia kazi  teknolojia inayotumia  nguvu ya akili bandia ya utambuzi inayojulikana kwa jina la  kujifunza  kwa kina, ambayo inatumia mifumo ya utambuzi wa seli za ubongo zinavyotambua mchakato wa data,Utaratibu ambao unaonekana kuisaidia Facebook kupata matangazo ya biashara kutokana na namna watumiaji wanavyowasiliana.

Ofisa wa Teknolojia wa Facebook Mike Schroepfer amesema lengo lingine la utaratibu huu ni kuweza kupunguza idadi ya mapachiko na habari zinazoonekana kwenye  mtandao huo kutoka 1500 kuwa 30 au 60 kwa zile ambazo ni muhimu tu.

Teknolojia hii pia kwa sasa tayali inatumiwa na makampuni ya google na microsoft ambapo inaelezwa ni miongoni mwa teknolojia 10 za hali ya juu zilizoibuniwa mwaka 2013.BBM SASA KUANZA KUPATIKANA KATIKA ANDROID NA iOSProgram Tumishi maarufu ya mawasiliano ya ujumbe wa papo kwa papo katika simu za BlackBerry inayojulikana kwa jina la  BlackBerry Messenger (BBM) inaanza kupatikana mwishoni mwa juma hili  katika vifaa vya mawasiliano vilivyotengenezwa katika mfumo wa program za  Android na  iOS.

Kampuni ya BlackBerry imesema program tumishi hiyo itapatikana katika vifaa vya mawasiliano vyenye Android 4.0 na zaidi ,  iOS 6 na iOS 7,ambapo itawawezesha watumiaji wa vifaa vya Android na  iOS kuwasiliana na wale wenye  BlackBerry.

BBM ni program tumishi inayowezeshwa na intanet kuwasiliana kwa ujumbe maandishi wa papo kwa papo na simu kwa njia ya video ambapo kwa sasa takwimu zinaonesha kuwa kwa mwezi watu milioni 60 wanaotumia BlackBerry wanajiunga na huduma hiyo.

 Pamoja na hayo kumekuwa na tetesi kuwa kampuni ya BlackBerry itapunguza asilimia 40 ya wafanyazi wake kutokana na kukosa soko kwa tabiti yake mpya ya PlayBook iliyotoka hivi karibuni.

Huduma za BBM katika  Android na  iOS

-Mawasiliano ya papo kwa papo katika simu za  Android, iPhone na  BlackBerry
-Ni zaidi ya kuchat-kwani unaweza kutuma file la sauti linaloambatana na maandishi.
-Unaweza kuwasiliana na watu wengi kwa wakati mmoja kwa idadi ya watu 30

-Inakupatia neno la siri la pekee linaloimarisha faragha kwa mtumiaji bila kutumia namba ya simu ama anuani yako ya barua pepe.

LINKEDIN YASHITAKIWA KWA KUINGILIA WASIFU WA WATUMIAJI
 
 

Watu wanne  huko nchini Marekani wameushitaki mtandao wa kijamii wa LinkedIn unaowaunganisha wanataaluma kuwa umekuwa ukiingilia wasifu wao kwa kutuma maombi  kwa marafiki zao kujiunga na mtandao huo. 

Tuhuma hizo zimeeleza kuwa  LinkedIn  imekiuka sheria ya shirikisho pamoja na sheria ya faragha ya jimbo la  California,ambapo imedaiwa kuwa  mtandao huo unapoomba anuani ya barua pepe kwa mtumiaji hauweki wazi kuwa  itatumika kuwaomba watu wengine kujiunga na LinkedIn kupitia anuani ya barua pepe ya mhusika.

Madai mengine yanayoelezwa ni kuwa kwa muda wa miaka mine watu wamekuwa wakilalamikia utaratibu wa masoko unaotumiwa na mtandao huo.

 Msemaji wa LinkedIn  Doug Madey  amesema kuhusu ulinzi wa faragha na data za watumiaji wa mtandao huo wa kijamii unaendesha kwa uwazi na madai hayo hayana msingi wowote. 

Friday, September 20, 2013

MASOMO KWA NJIA YA MTANDAO

Masomo kwa njia ya mtandao(Online Studies) kwa miaka ya hivi karibuni yamekuwa yakitolewa bure  na baadhi ya Vyuo Duniani. 

Mfano katika hiyo picha ni ni kozi ya takwimu, kutoka Chuo Kikuu cha Princeton.
 

Hata wewe waweza jiandikisha usome, kuna assignments na test, na mitihani, ukikamilisha vyote unapatiwa cheti.
bofya hapa coursera

VYUO VIKUU VYA UINGEREZA KUTOA ELIMU BURE KWA NJIA YA TEKNOHAMA
Vyuo Vikuu 23 nchini Uingereza kwa kushirikiana na taasisi 3 zinazojihusisha na masuala ya siasa na utamaduni wa nchi hiyo vimeanzisha mafunzo ya bure kwa watu wote duniani kwa kwa njia ya teknohama ( elimu mtandao) ambayo yataanza Oktoba 2013.

Utaratibu huo unaojulikana kwa jina la .future Learn utatoa mafunzo ya Ujasiriamali,Teknohama,Afya,Mazingira,Siasa,Sayansi,Usimamizi wa Biashara na  masuala ya kurekodi muziki,mafunzo hayo ni mwendelezo wa vyuo hivyo wa kutoa elimu masafa kwa kipindi cha miaka 40 iliyopita.

Mafunzo haya yatakuwa yakitolewa bure kwa njia ya mtandao kupitia kompyuta,tabiti na simu za mkononi zenye uwezo wa kupata intanet.

Kujiunga na mafunzo hayo bofya hapa futurelearn

Thursday, September 19, 2013

ICC YAWAONYA WANABLOG NCHINI KENYA

Mahakama ya kimataifa ya ICC imetoa onyo kali kwa wanablogu nchini Kenya,wanaotoa taarifa kuhusu mashahidi waliofika mbele ya mahakama ya ICC.

Hii ni baada ya taarifa kuhusu shahidi wa kwanza mbele ya mahakama hiyo kujitokeza kwenye mitandao hasa kwenye blogu, twitter na Facebook kumhusu.

Blogu hiyo ya udaku pia ilichapisha picha ya mwanamke huyo
Baadhi ya taarifa zilisema kuwa amewahi kutoa ushahidi wake ambao haukutofautiana na alioiambia mahakama ya ICC, katika mahakama nchini Kenya lakini ukapuuziliwa mbali na mahakama.

Mashahidi hao wanatoa ushahidi wao ndani ya mahakama ila wamefichwa nyuso zao hatua iliyochukuliwa ili kuwalinda kutokana na tisho lolote dhidi ya maisha yao.

ICC huenda ikachukua hatua za kisheria dhidi ya wanaosambaza taarifa kuhusu mashahidi wanaofika mbele ya mahakama hiyo.
Jaji anayeongoza vikao hivyo, Chile Eboe-Osuji, alisema kuwa ni makosa kisheria kuwafichua mashahidi wakati mahakama imebana kuwatambulisha.

Shahidi huyo ambaye wenye blogu wanasema wanamfahamu, ni mwanamke mwathiriwa wa shambulizi dhidi ya Kanisa la Kiambaa ambako yeye na wanakijiji wenzake walitafuta hifadhi wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi kutokota katika mkoa wa Rift Valley.

Watu zaidi ya thelathini waliteketezwa wakiwa hai ndani ya kanisa hilo.
Chanzo:BBC

Sunday, September 8, 2013

VIBER KWA WANAOTUMIA SIMU ZA ANDROID ANGALIA VIDEO HII

ANGALIA VIDEO YA JINSI YA KUWEKA NA KUTUMIA VIBER KWENYE IPHONE

Saturday, September 7, 2013

WASHINDI WA SHINDANO LA TWEET BORA ZA VITA DHIDI YA UMASKINI MWEZI AGOSTI WAPEWA ZAWADI

Embedded image permalink
Mwenyekiti wa IPP Reginald Mengi akitoa zawadi kwa washindi wa tweet bora kwa mwezi wa nane Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ardhi Lilian Wilson shilingi milioni moja,Suzana Senga laki 5 na  OmbeniKaaya laki tatu,Swali la tweet bora Septemba 2013 ni: Rasilimali za nchi hii zinawezaje kutumika kuongeza ajira kwa vijana ? waweza kutuma tweet ya majibu kwa @regmengi

FAHAMU KUHUSU TEKNOLOJIA YA VIBER-KUPIGA SIMU KWA BEI NAFUU

 

Viber ni teknolojia ya mawasiliano iliyoanzishwa kwa ajili ya mawasiliano ya papo kwa papo ya ujumbe wa sauti kupitia njia ya program tumishi ya sauti kupitia intaneti  VoIP kwa ajili ya simu za kisasa (Smartphone) na tabiti iliyobuniwa na Viber Media.

Pamoja na ujumbe wa mfupi wa maneno,watumiaji wanaweza kupigiana simu, kubadilishana picha,video na ujumbe wa sauti.Teknolojia hii yaweza tumika vifaa vya mawasiliano vinavyotumia progam tumishi zenye mifumo ya    Mac, Android, BlackBerry , iOS, Series 40, Symbian, Bada, Windows,Microsoft Windows Linux katika mitandao ya mawasiliano ya 3G/4G na Wi-Fi.

Takwimu zilizotolewa hivi karibuni na mtandao wa wikipedia zinaonesha kuwa mpaka kufikia Mei 7,2013 tayali watu milioni  200 million duniani wameshajiunga na Viber na tayali imeshaanza kutumika katika lugha 30 duniani.

 Viber  ilikubaliwa kutumika kwa mara ya kwanza katika  iPhone Disemba  2, 2010, ikiwa na ushindani na Skype.Baada ya hapo lilitolewa toleo jipya kwa simu za  Android mei  2011 lakini lilikuwa ni maalum kwa watumiaji  50,000 tu ndipo Julai 19,2012 lilipotolewa toleo la kutumiwa na watu wote 

 Viber kwa ajili ya BlackBerry na simu  Windows ilizunduliwa mei 8, 2012. Ambapo julai 24,2012 watu milioni 90 duniani  walikuwa wameshajiunga na teknolojia hii ya mawasiliano. million users on July 24, 2012,nakuongeza matumizi katika simu za  Android, iPhone, Nokia Series 40,Symbian na Samsung Bada

Mfumo wa mawasiliano wa sauti kupitia  Viber  katika simu za l Windows 8 ulianza kutumika  April 2, 2013.

Teknojia hii inakuwezesha mtumiaji kuwasiliana na mtu ambaye na  amejiunga kupitia namba yake ya simu ambapo unaweza kumpigia simu ikiwa simu zenu zinaina internet iwe ni katika nchi uliyopo ama nje ya nchi 


Viber Media ni kampuni iliyoko Cyprus ikiwa na vituo vyake Belarus na  Israel.Kampuni hii ilinzishwa na mmarekani mwenye asili ya Israeli mjasiriamali  Talmon Marco.


Kwa sasa kampuni hiyo haipatati mapato japo imetangaza kuwa itaanza kufanya hivyo mwaka 2013 kupitia matangazo ya biashara na mpaka kufikia mwezi mei mwaka 2013 jumla ya dola za kimarekani milioni 20 sawa na shilingi bilioni 30 za kitanzania zimeshawekezwa katika kampuni hiyo.


Kama unatabiti ama smartphone tafuta program tumishi inaitwa Viber ipakue na uiweke kwenye tabiti ama simu yako na fuata maelekezo,waweza tembelea hapa viber ama hapa viber.


.

TWITTER YAIFUNGA TENA AKAUNTI YA AL SHABAAB


 

Akaunti ya Twitter ya kundi la wanamgambo wa Al Shabaab imesitishwa kwa mara nyingine.
Ujumbe kutoka kwa Twitter katika akaunti yake ya @HSMPress1 ulisema kuwa akaunti hiyo imefungwa, ingawa hapakuwa na maelezo kwa nini hatua hiyo ilichukuliwa.

Katika taarifa iliyotumwa kwa shirika la habari la AFP kundi hilo lililaani hatua ya Twitter na kusema kuwa haitazaa matunda yoyote.

Mnamo siku ya Jumanne, Al Shabaab ilisema kuwa ilishambulia msafara wa magari ya rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud, ambaye hakujeruhiwa.

Hata hivyo habari hizo zilipuuzwa na ofisi yake ikisema kuwa rais hakujeruhiwa kwani kifaa kililipuka mbali sana na msafara wake.

Baadaye kundi hilo lilituma ujumbe kwa Twitter uliosema kuwa ,''Mara nyingine hautaponea ''kwa mujibu wa ripoti za , AFP. Hata hivyo akaunti yake ya kiarabu ingali iko wazi.
 
Kwa mujibu wa sera ya Twitter, akaunti zinazotumika kutuma vitisho,zinapaswa kufungwa. Akaunti pia zinaweza kufungwa ikiwa zinatumiwa kwa shughuli zisizo halali.

Taarifa ya Al-Shabab ilisema kuwa haina akaunti nyingine ya Twitter kwa kiingereza na kuwaonya watumiaji wa mtandao huo kuwa wajiandae kwa akaunti zao kuvamiwa.

Akaunti ya Twitter ya kundi hilo kwa jina @HSMPress, ilisitishwa mwezi Januari baada ya kundi hilo kuitumia kutuma ujumbe wa kutisha kuwa lingewaua mateka wa Kenya na kisha kusema kuwa limefanya hivyo.

Wadadisi wamesema kuwa katika siku za nyuma, Marekani ililazimisha Twitter kufunga akaunti hiyo ingawa haikuwa na nguvu za kisheria kufanya hivyo.

Hata hivyo Twitter inasema kuwa hakuna kitu kinachoweza kuzuia Al Shabaab kuwa na akunti nyingine baada ya nyingine za kwanza kufungwa.

Al-Shabab ilifungua akauti yake mara ya kwanza mwezi Disemba mwaka 2011 baada ya wanajeshi wa Kenya , kwenda Somalia kupambana na wanamgambo hao.

Wanamgambo hao wamefurushwa Mogadishu pamoja na kutoka miji mingine ingawa bado wanadhibiti sehemu nyingi za Kusini mwa Somalia.
Chanzo:BBC Swahili.

 

Wednesday, September 4, 2013

ANGALIA VIDEO YA TEKNOLOJIA YA NENO LA SIRI "PASSWORD"INAYOTAMBUA KWA MAPIGO YA MOYO WA MHUSIKA

Tuesday, September 3, 2013

MICROSOFT KUINUNUA NOKIA


Steve Ballmer mmoja wa maofisa wa Kampuni ya  Microsoft

Kampuni maarufu inayotengeneza programu za kompyuta, Microsoft, itanunua sehemu muhimu ya biashara ya kampuni ya kutengeneza simu za mkononi Nokia kwa kiasi cha euro bilioni 5.44. Katika tangazo la pamoja la makampuni hayo mawili juma hili, ilielezwa kuwa Microsoft itanunua kitengo cha huduma vifaa na huduma cha Nokia kwa euro bilioni 3.79, na pia hati miliki au hataza ya kampuni hiyo kwa euro bilioni 1.62.


 Katika makubaliano hayo, Microsoft itakuwa na haki ya kutumia huduma ya ramani ya kampuni ya Nokia. Makubaliano hayo, ambayo kwa mujibu wa wadau wake yatapanua mipaka ya mawasiliano ya simu za mkononi, yatakamilishwa mwanzoni mwa mwaka ujao. 


Katika makubaliano hayo, wafanyakazi 32,000 wa Nokia watahamia katika kampuni ya Microsoft. Aidha, makubaliano hayo yanamweka mkurugenzi mkuu wa Nokia Stephen Elop katika nafasi nzuri ya kuchukua nafasi itakayoachwa wazi na mkuu wa Microsoft Steve Ballmer ambaye atastaafu mwaka kesho.