OnlineWednesday, June 26, 2013

LAINI ZA SIMU AMBAZO HAZIJASAJILIWA KUZIMWA JULAI 10,2013

 
 
 
Laini za simu za mitandao ya simu nchini Tanzania ambazo hazijasajiliwa zitazimwa rasmi Julai 10, mwaka huu.

Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba alisema hayo Bungeni jana, ikiwa ni hatua ya kukabiliana na matumizi mabaya ya simu.

Alisema serikali pia imekamilisha kanuni na Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (Epoca) zitakazodhibiti matumizi mabaya ya simu za mkononi.
“Serikali pia inashirikiana na Jeshi la Polisi katika kuwasaka na kuwakamata wote wanaotumia simu vibaya,” alisema.

Makamba alisema Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) ilifanya usajili wa namba za watumiaji wa simu za mkononi ambapo hadi sasa namba za simu 24,399,000 zimesajiliwa.

 
“Usajili wa namba za simu pamoja na masuala mengine, ulikuwa na lengo la kupunguza matumizi mabaya ya simu za mkononi,” alisema.

Makamba wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mchungaji Getrude Rwakatare (CCM), ambaye alitaka kujua serikali inasema nini juu ya baadhi ya watu kutumia simu za mkononi kusambaza ujumbe mfupi na maneno ya kuzusha.
 

MAFUNZO YA TEKNOHAMA KWA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU TOKA GOOGLE HAYA HAPAKampuni ya Google imetangaza nafasi 30 za mafunzo ya teknohama katika kitengo cha matangazo kwenye mitandao ya intanet  kwa wanafunzi wa teknohama wa  vyuo vikuu toka nchi za  Ulaya,Mashariki ya Kati na Afrika yatakayofanyika katika ofisi za kampuni hiyo barani Ulaya zilizopo Dublin,Ireland kuanzi Septemba 22 hadi 25,2013.

Mafunzo hayo ambayo yatalipiwa kila kitu na kampuni hiuo yatahusu namna ya kuwajengea uwezo washiriki kutumia fulsa mbalimbali za kutangaza katika mitandao mbalimbali ya intaneti,kutana na wataalamu mbalimbali wa kampuni hiyo na ufahamu wa biashara mtandao.

Blog hii inaomba wanafunzi wa teknohama nchini Tanzania kutuma maombi kwa wingi,kwa melezo zaidi bofya hapa

Tuesday, June 25, 2013

TGNP YAKABIDHI VIFAA VYA MAWASILIANO KWA VITUO VYA TAARIFA NA MAARIFA


https://mail-attachment.googleusercontent.com/attachment/?ui=2&ik=b931c5dbcd&view=att&th=13f76744886931cb&attid=0.1&disp=inline&realattid=f_hibpxgn70&safe=1&zw&saduie=AG9B_P9SAGcEXozPwQsh5l_Uf5SP&sadet=1372143292431&sads=Xkb_wCjxSn7FAfcgZjqRh-JiZvA

https://mail-attachment.googleusercontent.com/attachment/?ui=2&ik=b931c5dbcd&view=att&th=13f76744886931cb&attid=0.2&disp=inline&realattid=f_hibpxgny1&safe=1&zw&saduie=AG9B_P9SAGcEXozPwQsh5l_Uf5SP&sadet=1372143357185&sads=0r2UQwXNiy8KMgKNjvyTI7Ha22Uhttps://mail-attachment.googleusercontent.com/attachment/?ui=2&ik=b931c5dbcd&view=att&th=13f76744886931cb&attid=0.3&disp=inline&realattid=f_hibpxgob2&safe=1&zw&saduie=AG9B_P9SAGcEXozPwQsh5l_Uf5SP&sadet=1372143434324&sads=T93WTY-qsiHajoqd3UAQYmLBmDc
Ofisa katika Kitengo cha Habari na Mawasiliano TGNP, Deogratius Temba, akikabidhi vifaa hivyo kwa wanakituo hicho.


Mtandao  wa Jinsia Tanzania (TGNP),  umepanua wigo wa mawasiliano kwa makundi ya pembezoni hasa wanwake kwa kuwapatia vifaa vya teknolojia ya habari na Mawasiano (TEHAMA) kwaajili ya kupashana habari katika Kituo cha taarifa na maarifa Mkambarani Morogoro Vijijini.


Akikabidhi vifaa hivyo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 1.9, Ofisa katika Kitengo cha Habari na Mawasiliano TGNP, Deogratius Temba, amesema kuwa  shirika hilo limeamua kutoa vifaa hivyo kwaajili ya kuhakikisha makundi yaliyoko pembezoni hasa wanawake wanafikiwa kwa kupata taairfa sahihi kwa wakati muafaka na kuwawezesha pia wao kutoa taraifa walizo nazo katika ngazi ya jamii.“Huu ni mradi unaowezesha sauti za jamii kusikika,  kuanzishwa kwa ‘Sauti ya Jamii’ kunawezesha  sauti za wanawake wengi kupewa taarifa na kutoa na kusikika, Tunajua hii itawezesha wanawake wengi  kupaaza sauti zao na kupambana na matukio ya ukatili wa kijinsia pamoja na changamoto nyingine zilizoibuliwa wakati wa Utafiti raghibishi mwaka 2012 na tamasha la Jinsia la mwaka 2012 hapa Mkambatani” alisema Temba


Alisema kuwa TGNP kwa muda mrefu imekuwa ikitumia TEHAMA kwa ajili ya mawasiliano, kuwafikia wadau mbalimbali, kujenga nguvu za pamoja   katika kuleta mabadiliko chanya.  Matumizi ya ujumbe mfupi wa simu  (SMS) imekuwa ni  moja ya TEHAMA ambayo  inatumika kwa wingi katika ngazi ya jamii. 

“Kwa mantiki hii TGNP imeona fursa kubwa ya kutumia ujumbe mfupi  kama nyenzo ya  kusaidia kuunganisha nguvu katika kuhabarishana na kuchukua hatua za kwajibisha  mamlaka na kuleta mabadiliko chanya” aliongeza.

Sauti ya jamii itatumia  teknolojia  ya bulk SMS yaani kutuma ujumbe  mfupi wa simu kwa kutumia computer kwa watu wengi zaidi ya 10,000 kwa wakati mmoja.  Sauti ya jamii  itasaidia  kupashana habari  kupitia kituo cha taarifa na maarifa cha jamii kwenda wa wadau mbali mbali wakiwemo wanaharakati waliohusika katika Utafiti wa mwaka jana, madiwani,  Wanajamii wa Mkambarani, kamati mbalimbali  za maendeleo Mkambarani,  viongozi wa serikali za mtaa , kata hadi wilaya, madiwani na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali. 
  

Makamu Mwenyekiti wa Kituo cha Taarifa na Maarifa Mkambarani, Teresia Berege, alisema kuwa kuwepo kwa Kituo hicho na vifaa hivyo vya kisasa kutasaidia  kurahisisha mawasiliano, upashanaji wa taarifa na kupata habari kwa haraka itakuwa ni ukombozi kwa watoto na wanawake na kuwaweka katika mazingira bora ya kupata maendeleo.Naye Diwani wa kata ya Mkambarani, danile Shawa alisema kuwa wanaharakati wa Mkambarani wanapaswa kutumia vizuri vifaa vilivyotolewa na TGNP ili vilete ufanisi na maendeleo kwa wakazi wa kata hiyo.

“ninawashauri mtumie vema hivi vitu, kwa hapa kwetu Mkambarani hii ni fursa ya pekee, tumepiga hatua sasa, tekonoljia ilikuwa nyuma sasa TGNP imewawezesha mnakwenda na wakati, mtumie vizuri kwa uaminifu na unagalifu na msitume taarifa ambazo hazina ukweli” alisema Diwani.
Chanzo:the habari

Saturday, June 22, 2013

MAKAMPUNI YA SIMU YASEMA YATAPANDISHA GHARAMA MWEZI JULAI,2013


 Kufuatia kuongezwa kwa kodi katika huduma za simu za mkononi , gharama za huduma hizo zinatajiwa pia kuongezeka kuanzia Julai Mosi 2013.
Taarifa ya pamoja iliyotolewa jijini Dar es salaam na Umoja wa Makampuni ya Simu za Mkononi Tanzania – MOAT imesema pendekezo la serikali la kuweka kodi ya 14.5 kwenye huduma za simu za mkononi hazitoweza kukwepesha kupanda kwa gharama za simu kwa watumiaji.

MOAT inasema awali kodi ilikuwa ikitozwa asilimia 12.5 katika huduma ya mawasiliano ya simu na kwmaba ongezeko la kufiikia asilimia 14.5 tofauti na nchi za jirani Kenya na Uganda ambazo zimeendelea kutoza viwango vya ushuru vya asilimia 10 na 12.5 tu ni mzigo kwa watumiaji wa huduma za simu za mkononi.

Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2013 unaainisha, huduma za mawasiliano kuwa ni; “huduma yoyote ya maelezo inayotolewa na makampuni ya mawasiliano ya simu kwa njia ya mawasiliano kwa kutoa au kupokea sauti, maandishi, na picha au taarifa ya aina yoyote kupitia mfumo wa kielektronikia.”Imesema taarifa hiyo iliyosainiwa na Vodacom, Airtel, Tigo na Zantel

MOAT imesema eneo mojawapo litakaloathirika ni huduma za Intaneti eneo ambalo linahitaji kuwekewa mikakati ya kulikuza kutokana na umuhimu wake katika maisha ya sasa kiuchumi na kijamii na wala sio kulizorotesha kwa kusababisha ongezeko la gharama na hivyo kuendelea kuwa na kiwango cha cha matumizi kilinganishwa na baadhi ya nchi nyengine zikiwemo za Afrika Mashariki.

“Hatua hii ya kuongeza kodi itakwenda kinyume na mipango iliyopo yenye lengo la kuibadili jamii kwa kuipatia maarifa ya msingi kupitia huduma ya intaneti sambamba na mawasiliano ya simu.”

Kwa mujibu wa MOAT, Tanzania ni kati ya nchi zenye kiwango cha chini ya matumizi ya huduma ya mtandao wa intaneti katika bara la Afrika ambapo watumiaji wa huduma hiyo ni asilimia 10 pekee ikilinganishwa na nchi jirani ya Kenya ambayo ina zaidi ya watumiaji asilimia 40.

Aidha, MOAT imeongeza kuwa, “mawasiliano ya simu si anasa bali ni huduma muhimu katika Tanzania ya leo, sasa tunawezaaje kuwatozakodi mara kwa mara watu hao hao ambao wanaitegemea huduma hiyo ili kuboresha maisha yao? Ilihoji taarifa hiyo ya MOAT.

Taarifa hiyo  imeendelea kusema kuwa kwa tozo la kodi ya mapato ya  asilimia 35 kwenye sekta hiyo ya mawasiliano ya simu linatosha kiasi ya kwamba sekta hiyo isngeweza kubeba mzigo zaidi wa ongezeko jingine.

Hivi sasa, upanuzi wa mawasiliano na miundombinu vijijini ndiyo kipaumbele cha sekta nzima. Tunaamini hapa ndipo ukuaji wa sekta ya mawasiliano ya simu itakapoonekana katika miaka ijayo. Ongezeko lolote la kodi litazorotesha uwezo wetu wa kutanua huduma zetu za mawasiliano na miundombinu maeneo ya vijijini, imesema MOAT.

“Tunaelewa kuwa serikali inayafanya haya yote ili kuweza kupata fedha kwa ajili ya kusaidia kwenye huduma za jamii katika maeneo muhimu. Ni bahati mbaya kwamba sekta ya huduma ya mawasiliano ya simu inaendelea kubeba mzigo mkubwa wa ongezeko hili ambapo wateja watalazimika kuubeba mzigo wa ongezeko hilo,” ilihitimisha taarifa hiyo ya MOAT.

Friday, June 21, 2013

TAKWIMU ZA WATUMIAJI WA MAWASILIANO KWA FACEBOOK BARANI AFRIKA HIZI HAPA

An overview of the latest user numbers in the largest Facebook markets across Africa.

Thursday, June 20, 2013

BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU TANZANIA YAZUNGUMZIA MATUMIZI YA M-PESA‏


BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU YAZUNGUMZIA MATUMIZI YA M-PESA‏
Mkuu wa Idara ya Mawasiliano, Habari na Elimu kwa Umma wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Cosmas Mwaisibwa akifafanua jambo wakati wa kikao baina ya bodi na kampuni ya Vodacom Tanzania kuangalia namna ya kuimarisha na kuboresha zaidi uhusiano wa biashara baina ya taasisi hizo mbili. Wengine pichani kutoka kulia ni Meneja Uhusiano wa Mambo ya Nje wa Vodacom Salum Mwalim na Naibu Mkurugenzi wa Tehama wa bodi Cuthbeth Simalenga.


Bodi ya mikopo ya elimu ya juu Tanzania  – HESLB imesema huduma ya M-pesa inayowawezesha waombaji wa mikopo ya elimu juu kwenye bodi hiyo kulipia ada ya uombaji kwa kiasi kikubwa imesaidia kurahisisha uendeshaji ikiwemo usimamizi na ufuatiliaji wa malipo hayo.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu nchini Bw. Cuthbeth Simalenga wakati wa kikao cha urafiki mwema kati ya uongozi wa Bodi na Kampuni ya Vodacom kilichofanyika makao makuu ya bodi hiyo yaliyopo Msasani Jijini Dar es salaam kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa taasisi hizo.


Bw. Simalenga amesema bodi hiyo ilianza kutumia huduma ya M-pesa kwa malipo ya ada ya maombi miaka mitatu iliyopita na kwamba tangu wakati huo huduma hiyo imekuwa ikiimarika na kutoa tija zaidi kwa upande wa uendeshaji wa shughuli za uombaji wa mikopo.


“Kwa miaka mitatu sasa tumekuwa tukitumia huduma ya M-pesa kukusanyia ada za malipo ya maombi ya mikopo, kwa sasa waombaji wote wanatumia huduma hii na tumekuwa tukiboresha mifumo yetu ya ndani mara kwa mara kukabiliana na changamoto za hapa na pale zinazojitokeza.”Alisema Bw. Simalenga


Zaidi ya waombaji 50,000 wakiwemo waombaji wapya na wale wanaaondelea na elimu ya juu hutuma maombi ya mikopo kwenye  bodi hiyo kwa mwaka, na wote kwa sasa wanatumia huduma ya M-pesa kulipia ada ya malipo ya maombi ambayo ni Sh 30,000.


Bw. Simalenga amesema changamoto kubwa inayowakabili kwa sasa katika mfumo huo wa malipo kuwa ni uaminifu wa waombaji hasa wanafunzi ambao baadhi yao hulalamika kushindwa kulipia au na kudai kutaka kurejeshewa fedha zao wakati huohuo wakiwa tayari wameshakamilisha mchakato wa uombaji na fedha hizo kupaswa kutumika kama ada ya uombaji.Chanzo:Habari Vyuoni

Wednesday, June 19, 2013

TWITTER YAENDELEA KUWA NA WATUMIAJI WENGI DUNIANI


 

Mtandao wa Kijamii wa Twitter unaendelea kupata umaarufu hivyo kuwa na watumiaji wengi duniani,taarifa iliyotolea hivi karibuni na tovuti ya mediabistro kutoka katika tovuti ya emaketer iliyotoa takwimu April,2013  inaonesha kuwa twitter imekuwa ikipata umaarufu zaidi nchini Marekani ambapo inakadiliwa kuwa na watu milioni 141.8 waliojiunga na mtadao huo hiyo ikiwa ni sawa na asilimia 27.4 ya watumiaji wa Twitter.

Pia imeelezwa kuwa Twitter inatumiwa na watu wengi huko Jamani na Uingereza na jambo la kushangaza ni kwamba mtandao huo unaonekana kupata umaarufu zaidi huko Indonesia ambapo kulikuwa na asilimia 44 ya watumiaji wapi waliojiunga na mtandao huo kwa mwaka 2012 ambapo watu milioni 30 walikuwa wamejiunga na mtandao huo wa kijamii.

Takwimu hizo zinaonesha kuwa huko Saudi Arabia asilimia 41.66 na Singapore asilimia 34.74 wanatumia twitter katika mawasiliano.

Takwimu za nchi 15 zenye watumiaji wengi wa mtandao wa kijamii wa Twitter katika mawasiliano duniani.

 


KUTANA NA BRCK,KIFAA CHA MAWASILIANO YA INTANETI KWA AFRIKA

Friday, June 14, 2013

BAJETI:HUDUMA ZOTE ZA SIMU NCHINI TANZANIA KUANZA KUTOZWA KODI MWEZI UJAO


 

Wamiliki wa simu nchini kuanzia mwezi ujao wataanza kuingia gharama zaidi kwa asilimia 14.5 ili kuongeza mapato ya Serikali na kugharimia elimu. 

Hayo yalisemwa bungeni jana na Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa wakati akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2013/14 unaoanza Julai Mosi, mwaka huu.

Akifafanua suala hilo kama chanzo kipya cha mapato ya Serikali, Dk Mgimwa alisema Serikali inakusudia kuanzia mwezi ujao kutoza ushuru wa bidhaa wa kiwango hicho kwenye huduma zote za simu za kiganjani, badala ya muda wa maongezi peke yake.

“Katika ushuru huu, asilimia 2.5 zitatumika kugharimia elimu hapa nchini... Hatua hii imezingatia mapendekezo ya Kamati Maalumu ya Spika ya Kushauri kuhusu mapato na matumizi ya Serikali,” alisema Dk Mgimwa.

Kama vile haitoshi, Waziri Mgimwa alitangaza kuongeza wigo wa kutoza ushuru wa bidhaa kwenye huduma za simu za mezani (zinazojulikana kama za TTCL) na zisizokuwa na waya.

Pia waziri alitangaza kuanzisha kodi ya zuio ya asilimia 10 ya kamisheni (commission) ya usafirishaji wa fedha kwa njia ya simu za mkononi. Kodi hiyo itakusanywa na kampuni za simu kutoka kwa wakala wanaotoa huduma za kusafirisha fedha kupitia simu za mkononi;

Mapendekezo hayo ya Waziri Mgimwa ni utekelezaji wa ushauri wa Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali, Ludovick Utouh kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), itafute vyanzo vipya vya kodi ili kuongeza mapato ya Serikali. 

Miongoni mwa maeneo ambayo Ripoti ya CAG iliyoishia Juni 30, mwaka jana ilishauri kuangaliwa, ni pamoja na huduma za kuhamisha fedha kwa njia ya simu za kiganjani maarufu kama M-Pesa, Tigo Pesa, Airtel Money na Easy Pesa.

CAG alishauri kuwa kampuni za simu kulipa kodi ya zuio ya malipo ya kamisheni inayolipwa kwa wanaofanya biashara hiyo na kodi hiyo ya zuio ipunguzwe kutoka katika kodi ya mwisho itakayotakiwa kulipwa na kampuni za simu.
Chanzo:Gazeti la mwananchi

PROGRAM TUMISHI YA WHATSAPP YAVUNJA REKODI


 whatsapp


Program tumishi ya WhatsApp inayotumika katika simu za mikononi kwa mawasiliano ya ujumbe mfupi Juni 13,mwaka huu  imetangaza imetoa huduma ya ujumbe mfupi bilioni  27 ndani ya masaa  24 ambayo ni mpya katika huduma ya ujumbe mfupi wa maneno katika simu za mikononi.
 Rekodi hii imevunja ile ya mwaka 2012 ambayo ilikuwa na ujumbe mfupi bilioni 19.

Kwa mujibu wa  Whatsapp, ni kwamba ujumbe mfupi wa maneno bilioni  10 uliopokelewa na watumiaji  bilioni  17, kumekuwa na uwiano wa ujumbe mmoja kutumwa kwa watu kumi kwa kutumia program hiyo. 

Whatsapp inayotumika katika simu za mkononi za  iOS, Android, Windows , BlackBerry, Asha, Symbian n.k kwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno,picha,audio na video imefanikiwa kuvunja rekodi yake,na kuweka ushindani na mitandao jamii ya Facebook na twitter katika kipindi cha miezi sita,ambapo kwa sasa Whatsapp inawatumiaji wapatao milioni 200.

Hatua hii imeonekana kuizidi huduma ya BBM inayotumiwa na simu za BlackBerry ambayo ndiyo iliyokuwa ikiongoza,ambapo kampuni hii toka Canada inawatumiaji milioni 60 wanaotuma na kupokea ujumbe bilioni 10 kila siku. 

Hata hivyo Whatsapp bado inaushindani kutoka sehemu mbalimbali  duniani ikiwemo Uchina ambako  kuna program tumishi ijulikanayo kwa jina la Wechat ambayo inawatumiaji milioni 300 kati ya hao milioni 40 wanaishi nje ya China.Wednesday, June 12, 2013

MAREKANI YADAIWA KUPEKUA MITANDAO DUNIANI

 

Shirika la Habari la Reuters limeripoti kuwa Wizara ya Sheria nchini Marekani imeanzisha uchunguzi kwa kile kinachosemekana ni ufichuaji wa taarifa za siri uliofanywa na mtaalamu wa zamani wa mitambo ya komputa katika shirika la ujasusi la Marekani,Edward Snowden.

Snowden alijitambulisha baada ya kufichua kuwa mashirika ya ujasusi nchini Marekani hufanya udukuzi kote dunini kwa kutumia mbinu ya kiteknolojia ya siri kuchunguza mawasiliano ya simu ya watu,barua pepe na mawasiliano mengine.

Ufichuzi wa Edward Snowden kuhusu shughuli hizo za kisiri zinazojumuisha kudukua mitandao na mawasiliano ya simu,umezusha wasiwasi kote ulimwenguni kuhusu kiwango cha ukusanyaji wa taarifa hizo za kijasusi Marekani.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza,William Hague,anatarajiwa kutoa tamko rasmi bungeni leo kuhusu tuhuma kwamba mashirika ya kijasusi ya Uingereza yalitumia data iliyokusanywa na mashirika ya kijasusi ya nchini hapo kubadili sheria kali kuhusu taarifa za siri.

Kwenye mahojiano na jarida la Guardian,Edward Snowden alisema kuwa wamarekani wanahujumu mamlaka ya serikali na kutishia demokrasia,hatua ya mtalaamu huyo wa teknohama imesababisha wasiwasi kuhusu uwezo wa Marekani kukusanya taarifa za kijasusi ambao anasema ni mkubwa.

Aliendelea kuliambia jarida hilo kuwa jambo inalofanya Marekani ni la kutisha,akiongeza kuwa wao huvamia mitambo na pindi mtu anapowasha mtambo wake wanaweza hata kuutambua mtambo wenyewe na mtu anayeutumia.

Saturday, June 8, 2013

KIJANA WA KITANZANIA ANAYEISHI SINGAPORE MWENYE MIAKA 14 ALIYETENGENEZA PROGRAM TUMISHI INAYOTUMIWA NA NOKIA

Saturday, June 1, 2013

TAARIFA KWA WATUMIAJI WA KASPERSKY ANTIVIRUS /INTERNET SECURITY 

Kumekuwa na matatizo kadhaa kwa watumiaji au wale wanaotaka kuweka bidhaa za kaspersky kwenye kompyuta zao .
Huu ni msaada mfupi wa kukabiliana na baadhi ya matatizo .

1 – WINDOWS 8
Kwa wale wanaonunua kaspersky antivirus au internet security kwenye maduka ya nchi za afrika mashariki wameona kwamba programu iliyopo kwenye cd haiwezi kuingia kwenye windows 8 , matukeo yake ni kutupa cd hizo na kutafuta antivirus nyingine .

Ni kwamba matoleo mengi ya kaspersky yaliyopo dukani sasa hivi
yalinunuliwa kabla windows 8 kutoka na hayana updates kwa ajili ya windows 8 .

Unachotakiwa kufanya kama unaweza tembelea tovuti ya kaspersky au
tovuti yoyote yenye programu mpya ya kaspersky utaweza kudownload bure utaingiza kwenye kompyuta yako na utaweza kutumia keys zile zile uliyonunulia antivirus yako .


2 – MAJIRA SAHIHI
Baadhi ya watu huwa wanaweka majira ambayo sio sahihi kwenye kompyuta zao ili kuepuka kushtukiwa kwenye masuala ya leseni kama za windows ,Microsoft office na nyingine nyingi .

Unapokuwa na majira ambayo sio sahihi kaspersky haitoingia au
haitofanya kazi kwa usahihi kwa sababu haitoweza kupata uwezesho
sahihi kutoka kwenye server ili iweze kuwa bora zaidi .

3 – MAHITAJI SAHIHI
Kaspersky haswa hii ya 2013 ni kubwa kitogo katika kuingiza na
ufanyaji kazi , kwahiyo inahitaji kompyuta kuwa na viwango sahihi ili kuweza kuingiza bidhaa hii na ili iweze kuwa nyepesi na ya haraka katika kutekeleza majukumu ya kulinda kompyuta yako .

Tafadhali angalia kompyuta yako kama inaviwango vinavyotakiwa na
kaspersky ili iweze kuingiza .

Mfano RAM inatakiwa iwe zaidi ya GB 1 ,

4 – UPDATES ILI KUBORESHA

Wengi wetu huwa tunajisahau kufanya updates za mara kwa mara kwenye kompyuta zetu haswa antivirus , matokeo yake ni kuvamiwa na virus au kushambuliwa na kuharibika kwa programu au kompyuta yenyewe .

Tafadhali unapopata kaspersky 2013 fanya updates kwa asilimia 100 muda huo kama unaweza , kisha uwe unaangalia updates za mara kwa mara ambazo zinaingia moja kwa moja .

5 – KUTUMIA ANTIVIRUS MBILI AU ZAIDI
Unaweza kutumia kama unajua kile unachofanya lakini sikushauri , pia sio antivirus zote zinakubali kuingia ambapo kuna moja nyingi
zitakuuliza kama unataka kuondoa moja ili hiyo unayoingiza iingie
nyingine hazina tatizo hilo .

Tatizo la antivirus ni kwamba hamna ambayo iko vizuri kwa asilimia 100 , nyingine zina matatizo Fulani katika utekelezaji wa baadhi ya majukumu au ni rahisi kushambuliwa na kuacha kufanya kazi .

Kwa ushauri zaidi kuhusu kaspersky au antivirus nyingine piga
0786 806028 au oldmoshi@gmail.com