OnlineMonday, August 6, 2012

WADAU WA KIPINDI CHA MAISHA NA TEKNOHAMA MORNING STAR RADIO

Kutoka Kushoto Gerald Masatu,Mtangazaji Maduhu,Brown Nyanza(IFM),Mama Kagize,Johnson Kuga Mzirai na Jonathan MnyelaJonathan Mnyela akifafanua katika kipindi cha maisha na teknohama ndani ya studio za Morning Star Radio jambo ambapo mada ilikuwa ni Kuifahamu Smartphone na Tables na jinsi zinavyoweza kuleta tija katika masuala ya maendeleo kwa wananchi

MASWALI NA MAJIBU KUHUSU UHARIFU KWA MITANDAO

Kumekuwa na ongezeko kubwa la uhalifu kwa njia ya mtandao kutokana na kukuwa kwa tekinolojia mbalimbali za mitandao na kuongezeka kwa maarifa kwa baadhi ya watu wanaofanya shughuli mbalimbali kwa njia ya mtandao , katika watu hawa kuna wema+ na wale ambao si wema wanaotumia ujuzi wao huu kwa ajili ya kufanya uhalifu mbalimbali .

MTANDAO NI NINI?
Ni muunganisho wa vifaa mbalimbali vya mawasiliano unaosababisha vifaa hivyo kuwasiliana au watu wanaotumia vifaa hivyo kuwasiliana kwa nia ya kupata taarifa , kuhifadhi , kuchapisha au kufanya shuguli nyingine yoyote kwa njia ya mtandao .
Mtandao ni sharti kuwe na muungano fulani, kama simu ya mkononi , kompyuta ,luninga za digitali na vifaa vingine mbalimbali.

UHALIFU KWA NJIA YA MTANDAO NI NINI?
Ni pale mtu au kundi la watu wanapotumia njia mbalimbali za kimtandao kutenda makosa , hii inaweza kuwa wizi kwa njia ya mtandao inaweza kuwa hela , wizi wa taarifa na masuala yanayohusiana na suala zima la wizi  , kudanganya watu watembelee tovuti Fulani kwa ajili ya kuwaibia taarifa zao , kuchapisha taarifa za uwongo ,kudownload (kupakua) program au muziki bila kununua au kwa kutumia program zilizokatazwa ,kutokufuata sheria na taratibu za nchi au eneo husika pale tunapotumia mtandao unapokuwa hapo .

UHALIFU WA MTANDAO UNA MIPAKA?
Uhalifu wa mtandao una mipaka kutegemeana na sheria au taratibu za sehemu ambayo mtu anatumia kwa wakati huo , kwa mfano kuna baadhi za nchi sheria zake za mtandao haziruhusu kutembelea au kutafuta vitu Fulani kwa njia ya mtandao ukifanya hivyo unakuwa umefanya kosa ,lakini uhalifu unaweza kufanyika mtu akiwa popote na saa yoyote endapo ameunganishwa kwenye mtandao .

SHERIA ZINASEMAJE KUHUSU UHALIFU WA MTANDAO?
Kama nilivyosema inategemea na mtu alipo na jinsi uhalifu ulivyofanyika , kuna baadhi ya nchi hazina sheria za masuala ya mitandao haswa inayohusu mawasiliano ya kimataifa(Internet), mtu anapokuwa kwenye nchi hiyo akafanya uhalifu sehemu nyingine ni ngumu kumtia hatiani au sheria za nchi husika zinapokuwa sio nzuri zinavutia zaidi wahalifu kujihifadhi au kutumia mitandao ya nchi hiyo kufanya uhalifu dhidi ya maeneo mengine ya dunia .

TANZANIA NA AFRIKA MASHARIKI TUKO WAPI ?
Mpaka sasa hakuna sheria moja ya masuala ya mawasiliano kwa jumuiya ya afrika mashariki kila nchi ina sheria zake ndogo ndogo Kwa Tanzania kuna EPOCA ambayo inagusia zaidi mawasiliano ya elekitroniki ,na kuna kikundi cha kupambana na uhalifu kwa njia ya mtandao kinachoitwa CERT .

SASA TUFANYAJE?
Nchi inapokuwa na sheria zake za mawasiliano haswa ya mtandao inapendeza na wengine haswa kampuni zinaweza kuandaa sera zao za mawasiliano kutumia muongozo wa nchi husika , sasa hivi kwa kampuni na mashirika hapa Tanzania yamekuwa yanapata tabu kuandaa sera zao za mitandao kutokana na kukosekana kwa sheria hizi za nchi .
Hata kama nchi haina , wewe kama kiongozi wa sherika au kampuni unaweza kuandaa muongozo wa mawasiliano ndani ya idara yako au kampuni yako itakayoongoza wafanyakazi na wageni wengine wanaotumia vifaa vya kazini kwako kwa ajili ya mawasiliano ili waweze kufuata taratibu na wanaweza kujiepusha na uhalifu mbalimbali kwa njia ya mtandao .

Miongozo hii inahusiana na matumizi ya vifaa pale anapoanza kutumia mtandao au anapoleta vifaa vyake kuunganisha , au anapotoa maoni katika mitandao ya kijamii , kuangalia picha , kushusha  vitu mbalimbali , haki miliki na mengine mengi.

Na: Bupe Berrums bberrums@gmail.com-Wanabidii