OnlineMonday, October 31, 2011

KARIBU KATIKA BLOG YA KIPINDI CHA REDIO CHA MAISHA NA TEKNOHAMA

Baadhi ya watayarishaji wa kipindi cha Maisha na Teknohama Masatu G.M,Johnson Kuga na Maduhu Emanueli
Maisha na Teknohama ni kipindi kinachosikika kila jumapili saa 3 asubuhi hadi saa 4 asubuhi kupitia 105.3 FM Morning Star Radio jijini Dar es salaam,
Kipindi hiki kilichoanzishwa mwaka 2007 na Maduhu Emanueli J.S,Johnson Kuga na Godfrey Jonathan waliokuwa wakisoma Teknohama katika chuo kimojawapo hapa Dar es salaam,kipindi hiki hutoa elimu,maarifa na habari mbalimbali kuhusu Teknolojia ya Habari na mawasiliano,watayarishaji wa kipindi hiki kwa sasa ni Maduhu Emanueli,Masatu G.M,Jonathan Mnyela na Johnson Kuga

Blog hii itakuwa ikikufahamisha habari mbalimbali kuhusu kipindi hicho na maarifa mbalimbali kuhusu teknohama pia tunapenda kushirikiana nawe kwa kutuandikia habari za kiteknohama kupitia maduhu@gmail.com ama kushiriki nasi katika kipindi kama ilivyoelezwa hapo juu.