OnlineWednesday, August 9, 2017

MFUMO MPYA WA ULIPAJI KODI YA PANGO LA ARDHI NCHINI.


 
      Wataalamu kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakitoa elimu jinsi ya kutumia mfumo wa Government electronic Payment Gateway kwa watendaji wa Halmashauri ya Kinondoni.
 
Elimu ya jinsi ya kutumia mfumo mpya wa kielektroniki ikitolewa kwa watendaji wa manipaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Watendaji wa Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Kinondoni wakipewa mafunzo jinsi mfumo mpya wa ukusanyaji maduhuli ya Serikali utakavyokuwa unatumika.
 Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeanza rasmi kutumia mfumo wa kielektroniki wa Government electronic Payment Gateway (GePG) katika makusanyo ya kodi ya pango la ardhi pamoja na tozo nyingine zinazotokana na sekta ya ardhi nchini.
Mfumo huu utamrahisishia mwananchi kulipa kodi ya pango la ardhi popote alipo, ikiwa ni pamoja na kulipia tozo nyingine mbalimbali za sekta ya ardhi. Pia mfumo wa GePG, utamuwezesha mwananchi au mmiliki wa kipande cha ardhi, kujua anadaiwa kiasi gani cha kodi ya pango la ardhi na kulipia popote alipo bila kusumbuka kufuata huduma hizo katika vituo vya makusanyo.
Majaribio ya ukusanyaji kodi ya pango la ardhi kwa kutumia mfumo wa kielektroniki yalifanywa katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, baada ya mafanikio makubwa kuonekana elimu ikatolewa kwa watendaji wote wa sekta ya ardhi katika Halmashauri zote za mkoa wa Dar es salaam kabla ya zoezi hilo kuhamishiwa mikoani.
Mwananchi yeyote anayemiliki kiwanja au shamba lililopimwa na kuwa na hati, ataweza kutumia simu yake ya mkononi kujua kiasi cha kodi ya pango la ardhi anachodaiwa na kukulipa kwa kutumia simu yake ya mkononi pia.
Kwa zile huduma nyingine za sekta ya ardhi ambazo zinahusisha malipo kama vile upekuzi katika daftari la msajili (official serach), mwananchi atapaswa kutembelea ofisi za Wizara ya ardhi zilizo katika eneo lake na kupatiwa makadirio ya kulipia huduma husika pamoja na namba ya malipo itakayomuwezesha kulipia aidha kwa njia ya benki au simu ya mkononi.
Kwa sasa kikosi kazi kinachotoa mafunzo juu ya matumizi ya mfumo huu kimeshaanza kuelemisha mikoa mingine baada ya kupata mafanikio mazuri katika mkoa wa Dar es Salaam. Lengo kubwa la kutumia mfumo huu ni kuongeza ufanisi katilka ukusanyaji wa maduhuli ya serikali pamoja na kurahisisha ulipaji kodi ya pango la ardhi nchini,

Monday, August 7, 2017

MAAMUZI TOKA KWA MKUTANO WA GAiN 2017 BRAZIL


 Image may contain: 30 people, people smiling, people standing, shoes and indoor

Mkutano Mkuu wa Mifumo ya utunzaji na usimamizi wa washiriki wa Kanisa la Waadventista wa Sabato Ulimwenguni umemalizika katika jiji la Sao Paulo, Brazil Agosti 6 2017 ukiwa umefanya maazimio yafuatayo.

1. Taarifa rasmi na sahihi za idadi ya washiriki wa kanisa zitapatikana kupitia mfumo wa ACMS pekee.

2. Anwani za makanisa yote ya Waadventista zinapaswa zipatikane kupitia mfumo wa ACMS

3. Kila mwezi karani wa kanisa atatuma taarifa ya washiriki kwenda konferensi, ambayo itaendelea kutumwa mpaka ngazi ya juu.

4. Division ya Amerika kusini inajaribiwa na mfumo mpya wa 7ME ambao unaruhusu kila mshiriki kujaza takwimu zake mwenyewe na ukifanikiwa ndio utatumika rasmi ulimwenguni kote ifikapo mwaka 2018.

5. Idara zote za kanisa zitatumia mfumo wa ACMS kutoa taarifa za idara.

Mkutano huu ulikuwa na wajumbe 31 kutoka ulimwenguni kote na Divisheni ya Afrika Mashariki na kati iliwakiliswa na wajumbe wawili

Friday, June 9, 2017

TEKNOHAMA YAKUZA UFANISI MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BANDARI TANZANIA (TPA)


Serikali Mtandao inarahisisha utendaji kazi na utoaji wa huduma kwa umma. Usikose kuangalia kipindi hiki cha Seikali Mtandao katika Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) uone jinsi wanavyotumia mifumo mbalimbali ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika kazi zao za kila siku.

Thursday, June 8, 2017

INTANETI INAVYOCHOCHEA UKUAJI WA UTALII BARANI AFRIKA

Afrika ni Bara la pili kwa kuwa na idadi kubwa ya watu ambapo inafikia takribani bilioni 1.2 (wengi wao wakiishi mijini) na inatarajiwa kongezeka mpaka bilioni 2.5 kufikia mwaka 2050 (25% ya watu wote duniani).

Kwa mujibu wa ripoti ya utalii kwa Afrika mwaka 2017 iliyofanywa na Jumia Travel imebainisha kwamba mtu mmoja kati ya watatu ni sehemu ya watu wa daraja la kati (watu wanaofanyakazi kwenye taaluma na biashara mbalimbali pamoja na familia zao) na wanatarajiwa kuongezeka mara mbili zaidi kufikia 2050. Watu wa daraja la kati ni muhimu katika uchangiaji wa ukuaji wa utalii wa ndani na ukanda mzima tuliopo.

Saturday, May 13, 2017

MAELFU YA KOMPYUTA YADUKULIWA NA KUTEKWA NA KIRUSI CHA 'WANACRYPT'


 https://4.bp.blogspot.com/-y9y5x_KYGJI/WRaROuNbylI/AAAAAAAASZo/zrgXaLrY46oH-m6tzRzPD4mR2NRj0uOiQCPcB/s320/27.jpg
Maelfu ya tarakirishi (kompyuta)  za mitandao ya mashirika makubwa kadhaa duniani yamedukuliwa  na kutekwa na watekaji wanadai malipo ili kuwarudishia wenye mitandao hiyo. 

Udukuaji huo umetumia program ya udukuaji iliyotengenezwa na shirika la usalama wa taifa la Marekani (US National Security Agency-NSA) ambalo nalo lilibiwa program hiyo na wajanja. 

Wadukuaji  hao wanaojiita The Shadow Brokers ndio wanaodai kuwa waliiba program hiyo na kuiweka hadharani katika mitandao ya internet. 

Kampuni ya Microsoft ilitengeneza ngao ya kuzuia udukuaji kwa kutumia program hiyo na kuiweka hadharani mwezi Machi, lakini ni wazi watu wengi hawakutumia nafasi kuweka ngao hiyo.  

Kampuni mbalimbali kutoka nchi 99 zinasemekana mitandao yao imetekwa, kumekuwa na malalamiko kutoka Uingereza, Marekani, China, Urusi, Hispania, Italia,Taiwan na nchi nyingi nyingine.

 Kampuni ya ulinzi wa mitandao (Cyber-security) ya Avast imesema imeweza kupata malalamiko 75,000 ya madai ya kuhusu kirusi cha WannaCrypt, kutoka karibu pande zote duniani. 

https://3.bp.blogspot.com/-Ftp2EPbigA4/WRaqdlxnQhI/AAAAAAAASaQ/GaiuWfAeQ4EGAJd1XdI-cWOVADS1aDlIACLcB/s1600/_96034173_cryptor3.png
Hivi ndivyo kompyuta inavyosomeka ukishadunguliwa na kirusi cha Wannacry
Kati ya waliokumbwa na kadhia hii ni Taasisi ya Afya ya Uingereza (National Health Service), hali ambayo imeleta mkanganyiko mkubwa katika hospitali za nchini Uingereza, miadi imevurugwa, wagonjwa wamerudishwa nyumbani, waliokuwa wafanyiwe upasuaji shughuli zimeahirishwa kwani maelezo yote yako kwenye kompyuta na hazisomeki. 

Urusi imesema imeweza kugundua chanzo na inakishughulikia. Huko Ujerumani kampuni ya kuuza tiketi za treni imekubwa na kadhia hiyo wakati maabara ya chuo kikuu kimoja Italy imekutana na tatizo hilo. 

Spain imejikuta ikipata tatizo hilo kwenye kampuni yake kubwa ya simu ya  Telefonica, kampuni ya umeme ya Iberdrola na kampuni ya kusambaza gesi ya Gas Natural, wafanyakazi wa kampuni hizo walielekezwa kuzima kompyuta zote. 

Kampuni ya simu ya Portugal Telecom, na kampuni ya kusafirisha mizigo ya FedEx, ofisi moja ya serikali ya mtaa huko Sweden na kampuni ya simu za mkononi ya Megafon ya Urusi ni kati ya wahanga wa tatizo hili.

 Nani hasa waliosababisha hili? Wataalamu wengine wanasema wahusika inawezekana waligundua mapungufu katika program ya Microsoft, NSA waliliona hilo pia na walitengeneza program iliyokuwa inaweza kuteka kompyuta zote zinazotumia Microsoft, program hiyoikaibiwa na wezi wanaojiita (The Shadow Brokers), wezi hawa walianza kuinadi program hiyo katika mtandao na hatimae tarehe 8 April 2017, wakaigawa bure kwa kusambaza password mtandaoni. Wakidai wamefanya hivyo kama njia yao ya kumpinga Rais Donald Trump. 

Microsoft tayari wameshatengeneza program ambayo itakuwa inaweza kutoa taarifa kama kompyuta yako imeingiliwa na udukuzi wa WannaCrypt.
CHANZO:theiringa.blogspot.com